Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Wakufunzi wa afya na maabara, wauguzi na madaktari wametakiwa kujiendeleza kielimu kwa kuchukua mafunzo ya Afya yanayotolewa katika taasisi ya serikali ya Cedha ili kwendana na uwekezaji mkubwa wa sh,trilioni 6.7 uliofanywa na serikali katika sekta hiyo.
Rai hiyo imetolewa na Ofisa Ustawi wa jamii mkoa wa Arusha,Denis Mgiye wakati alipomwakilisha mganga mkuu wa mkoa,katika ufunguzi wa mafunzo ya afya kwa taasisi 16 za serikali, watu binafsi na mashirika ya kidini.
"Nikipongeze chuo cha Afya cha Cedha kwa sababu kimekuwa mdau mkubwa wa kunoa wataalamu wa afya na mnajukumu kubwa la kutuandalia wataalamu bora wa Afya lengo ni kuhakikisha sekta ya afya ina kuwa na rasilimali watu salama"
Mgiye alisema katika mkoa wa Arusha serikali imewekez kiasi cha sh, trilioni 12 kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya afya katika hospitali za rufaa,wilaya ,vituo vya afya na zahanati na kuwataka wataalamu wa afya kujiendelea ili ujuzi watakaoupata wautumie kusaidia jamii kuondoa changamoto changamoto za afya katika maeneo yao.
Alisema kwa upande wa vifaa tiba vya afya serikali imewekeza kiasi cha sh,bilioni 2.5 ili kurahisisha upatikanaji wa vifaa tiba na mazingira mazuri ya utoaji huduma.
Awali mkuu wa taasisi ya Afya ya Cedha, Dkt Johannes Lukumay alisema taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya watumishi wa Afya Arusha, Cedha inayomilikiwa na wizara ya afya .
Alisema ilianzishwa mwaka 1983 kwa malengo makuu manne ikiwemo kuwafundisha wakufunzi wa vyuo vya taaluma za Afya mbinu za ufundishaji na upimaji.
Pia kuwaendeleza kitaaluma watumishi wa sekta ya afya waliopo kazini ,kufanya tafiti zenye kutatua changamoto sekta ya afya na kutoa ushauri elekezi kuhusu masuala ya afya.
Alisema jumla ya wakufunzi wapatao 31kutoka vyuo mbalimbali vya afya nchini vikiwemo vya serikali, vyuo binafsi na vyuo vya mashirika ya dini wanashiriki mafunzo hayo ya siku 11 kwa lengo la kuwaongezea ujuzi namna ya kufundisha taaluma hiyo..
Alisema mafunzo hayo yatawaongezea uelewa juu ya utahili wa kisasa wa kupima wanafunzi kitaalamu, pia watajifunza njia sahihi za utunzaji wa maswali na jinsi ya kutahili wanafunzi.
Aidha dkt Lukumay alisema pamoja na jitihada kubwa za chuo kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ,changamoto kubwa ni idadi ndogo ya washiriki ,ambapo aliwaomba wadau wa afya kuendelea kuitangaza taasisi hiyo ya serikali ili kuendelea kutoa huduma hiyo kwa idadi kubwa zaidi ya washiriki .
Ends.....
0 Comments