Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Maharage Chande amesema shirika hilo linaendelea kutumia teknolojia ya TEHAMA katika kufanya biashara mtandao (E-Comas) ili kukidhi ushindaji wa bidhaa katika ukanda wa Afrika na Dunia kwa ujumla.
Hayo ameyalsema jijini Arusha wakati wa maadhimisho ya miaka 44 ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Maharage Chande, alisema Shirika la Posta hivi sasa linafanya mabadiliko makubwa ya kuboresha huduma zake ili kuendana na kasi ya teknolojia ambaho inakua kwa kasi.
"Tunatekeleza sera na mipango ya nchi katika kukuza biashra mtandao ambayo inajumuisha usafirishaji wa vipeto kwa njia ya haraka ambapo timeshafungua vituo vya utimilifu Arusha,Zanzibar,Dodoma na Dar es Salaam ili ndani ya siku mbili mtu akiwa sehemu yoyote duniani anapokea mzigo wake,",alisema
Aidha alisema hivi sasa wapo kwenye mpango wa kuanzisha huduma ya 'Money oder' ambayo inatoa huduma ya kifedha kwa gharama nafuu kwa wanachama wake.
"Miaka kumi iliyopita tulikua tunafanya bajeti kubwa ya uuzaji wa ndanibya mabango makubwa ili tuwafikie wateja wengi wanaotumia zaidi huduma zetu lakini leo mambo yamebadilika tukitumia tweet moja tu inawafikia mamilioni watu kwahiyo na siso shirika la Posta lazima tubadilike kulingana na mabadiliko ya kidjitali yanayoikumba Dunia nzima,"alisema.
Kaimu Katibu Mkuu Selestine Kakole alisema wanajivunia kama nchi kutimiza ndoto ya waasisi wa bara la Afrika kwa kuwezesha upatikanaji w ajengo hilo la makao makuu ya PAPU barani Afrika.
"Kutekeleza majukumu ya kisera na kibiashra katika mashirika ya posta kwa nchi za Afrika ni jambo muhimu lakini kuna mambo chanya yanayoathiri utoaji wa huduma lakini ni lazima twende na wakati kwa kuwekeza kwa kasi ili tusiachwe na teknolojia na utoaji huduma ya kibiashara kwa njia ya mtandao,"alisema.
Alisema serikali inajikita katika kuweka mikakati kuhusu teknolojia za muundo wa ecommerce ili kuhudumia wananchi wengi zaidi.
Waziri wa Habari, Mawasiliano Teknolojia na Posta, kutoka nchini Zimbabwe Dk.Tatenda Annastacia Mavetera alisisitiza PAPU kuweka mikakati thabiti inayoendana na kasi ya kidijitali inayowezesha kuvuta zaidi wafanyabiashara kutumia huduma zao.
"Tunataka kuona PAPU inasonga mbele katika uwekezaji wa posta ya kidijitali pamoja na kukuza biashara mtandao katika ukanda wa Afrika," alisema.
Mwisho
0 Comments