KIONGOZI WA DINI ARUSHA ATEMA NYONGO MAANDAMANO YA CHADEMA,AMPONGEZA RAIS SAMIA ,AMTAKA KUKAA MEZA MOJA NA UPINZANI KUONDOA TOFAUTI ZA KIITIKADI,AITAKA SERIKALI KUTOA MAJIBU KUPANDA BEI KWA BIDHAA

  Na Joseph Ngilisho Arusha


Kiongozi wa dini Mkoa wa Arusha ,Sheikh Haruna Husein,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha demokrasia hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuruhusu Maandamano ya amani ya chama cha upinzani jambo linaloonesha  ni ukomavu wa kisiasa.


Aidha Sheikh Haruna ,aliwaomba viongozi wa serikali kujenga desturi ya kukaa meza moja na viongozi wa vyama vya siasa ili kufikia mwafaka wa masuala mbalimbali wanayotofautiana kuliko kusubiri maandamano ambayo sio njia sahihi sana ya kumaliza changamoto hiyo.


Kiongozi huyo wa dini ameyasema hayo jana wakati akiongea na vyombo vya habari jijini hapa, kuhusiana na hali ya demokrasia hapa nchini pamoja kupanda kwa bidhaa mbalimbali  na kuitaka serikali ihakikisheni bei ya vyakula inashuka ili kuwapunguzia ukali wa maisha kwa watanzania hususani wenye kipato kidogo,( wanyonge).


"Kitendo cha rais Samia kuruhusu wapinzani kuandamana ni kuonesha ukomavu wa taifa hii la Tanzania, hatua hii imeepusha hata uvunjifu wa amani iwapo kama wangekatazwa na wao kulazimisha kuandamana ,sisi kama viongozi wa dini tumeona ni hatua nzuri ya ukomavu wa kisiasa lakini sio njia sahihi ya kutatua changamoto"


Haruna alisema pamoja na kwamba maandamano ni haki ya msingi ya kikatiba ,haoni sababu ya kufikia hatua hiyo wakati kuna wigo mpana wa kukaa meza moja na kufikia mwafaka wa kidpromasia jambo litakaloepusha muda na usumbufu wa watu kushinda wakitembea na kufanya shughuli za uzalishaji kusimama.


"Wale wenye fursa ya kukaa meza moja na serikali wapewe nafasi ,hatuwezi kuipata kwa kutembea barabarani na hii ndio  msimamo wangu kama kiongozi wa dini ni lazima tukae na rais tumwambie changamoto zetu na nyie serikali shusheni bei ya bidhaa kama sukari na mafuta ili kuondoa hizi kelele"


"Sisi kama viongozi wa dini tunampongeza sana rais samia kwa kuruhusu demokrasia ikiwe mo kukosolewa kwa njia ya maandamano ya amani ila tunasema sio njia sahihi sana ya kuondoa changamoto, njia bora yenye tija ni kukaa mezani"


Naye sheikh wa taàsisi ya  Twarika,  Iddy Ngela alisema ni hatua kubwa kwa serikali ya rais Samia kuruhusu  Maandamano ya amani yaliyofanywa na chama cha upinzani kwani ni nchi chache sana duniani ninazoweza kuruhusu kukosolewa kwa njia hiyo.

 

"Rais amepanua wigo wa demokrasia hapa nchini vyama vingi vya kisiasa hapa nchini vimepewa fursa ya kikatiba kufikisha ujumbe wao kwa amani ya maandamano pasipo kuvunja sheria hii ni hatua kubwa kwa taifa la Tanzania"


Alisema rais Samia amefanikiwa kupuuza kauli ya chama tawala cha ccm ambayo imekuwa ikitolewa na baadhi ya wanasiasa kuwa vyama vya upinzani ni vyama vya vurugu na havipaswi kupewa nafasi kuandamana ila kwa hatua hii imeonesha jinsi gani rais wetu samia amekomaa kisiasa. 


Ends..

















Post a Comment

0 Comments