KATA YA THEMI YAONJA MATUNDA YA RAIS SAMIA, MILIONI 200 KUJENGA JENGO LA MAMA NA MTOTO, KINABO AAHIDI UJENZI KUANZA MWEZI UJAO, FEDHA ZIMEINGIA!

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

 Wakazi wa kata ya Themi na viunga vyake katika jiji la Arusha wanatarajia kuondokana na adha ya akina mama kukosa huduma ya kujifungulia mara baada ya serikali kupitia halmashauri ya jiji la Arusha kutoa kiasi cha sh milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto .


Akiongea na vyombo vya habari mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa kituo cha afya cha Themi ,Melace Kinabo alisema fedha hizo zimetolewa na Rais Samia Suluhu kutokana na kilio cha muda mrefu cha wananchi wa kata hiyo kukosa huduma ya kujifungua na upasuaji. 



"Katika kata yetu ya Themi kumekuwepo na changamoto kubwa ya muda mrefu kwa wanawake kukosa huduma ya  kujifungua kiasi kwamba  iliwalazimu kuhama makazi ili kusogea karibu na huduma ,ila kwa sasa tunamshukuru sana rais Samia kwa kulitambua hilo na kutoa kiasi hicho cha fedha kupitia jiji la Arusha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto litakalokuwa na wodi ya wazazi na chumba cha upasuaj".


Mwenyekiti huyo alisema kuwa mchakato wa ujenzi wa jengo hilo wameuanza miaka mitatu iliyopita na wanashukuru kupata sapoti ya serikali kwa sababu changamoto za kujifungua zilikuwa ni kubwa kutokana na umbali wa kufuata huduma hiyo.


Alisema katika kikao walichoketi, kamati hiyo wamekubaliana kwamba siku za usoni wanatarajia kuanza mchakato wa ujenzi ikiwemo kutangaza tenda na wamepanga ifikapo Machi mwaka huu ujenzi wa jengo hilo uwe umeanza mara moja.


"Fedha hizo tayari zimeshaingia kwenye akaunti ya Kituo na leo tumefanya kikao za maamuzi namna ya kutumia fedha hizo na tumekubaliana matumizi sahihi  ya fedha z serikali na hatutachelewesha mradi huo na tutakuwa tukishirikiana na jiji la Arusha ili kuharakisha mradio huo"


Kinabo aliwaambia wananchi wa kata hiyo hususani akina mama kuwa wavumilivu wakati mchakato wa ujenzi unafanyika na wanatarajia ifikapo  katikati ya mwaka huu jengo hilo liwe limekamilika  .


Naye mjumbe wa kamati hiyo Catherine Nyabamba ambaye pia ni katibu mwenezi wa ccm kata hiyo, aliishukuru serikali kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa jengo hilo kwani litaokoa maisha ya akina mama wanaojifungua ambao hapo awali walipata changamoto kubwa.

Alisema wananchi watanufaika na mradi wa jengo hilo  pindi litakapokamilika na kuwapunguzia gharama walizokuwa wakizitumia wakati wa kuwapeleka akina mama kupata huduma za kujifungua hasa nyakati za usiku.


Naye mkazi wa eneo hilo Juliana Laizer alimshuku sana Rais Samia kwa kuwapatia fedha hizo na kuelez kwamba wanajivunia serikali ya rais samia kuwajali akina mama na mtoto jambo litakalosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.


Ends....











Post a Comment

0 Comments