KANISA LAWAKUMBUKA YATIMA,WAJANE NA WAGANE,ASKOFU ATEMA CHECHE OLE WAO WANAODHULUMU WAJANE,ATOA MAAGIZO MAZITO KWA VIONGOZI WA SERIKALI

 Na Joseph Ngilisho Arusha  


Kanisa la Kinabii la Naivera (Naivera Church  Apostolic) lililopo Ungalimited jijini Arusha,limewapatia msaada wa vyakula na vitu mbalimba watoto yatima ,wajane na wagane wapatao 349 ikiwa ni utaratibu wa kila mwaka wa kanisa hilo kusaidia makundi yenye uhitaji.

Akizungumza katika hafla ya chakula , iliyoandaliwa na kanisa hilo kwa ajili ya makundi hayo maalumu  , Askofu Mkuu wa Makanisa ya Naivera, Dkt Julius Laizer alisema ni jukumu la kanisa hilo kuwajali na kuwapatia msaada watu wasio na uwezo, linalofanyika kila mwaka kwa lengo la kuwafariji.




Alisema wajane na yatima wanapaswa kulindwa na kuonewa  huruma.Askofu huyo aliwaomba viongozi wa serikali  wasimame imara kuyatetea makundi yasio na uwezo kwa kuwa wanastahili kuishi kama watu wengine. 

Alizitaja changamoto kadhaa zinazochangia uwepo wa makundi hayo ni pamoja na ugomvi wa kifamilia ikiwemo manyanyaso , Kudhalilishwa kingono ,kubaguliwa na kutengwa ,ugomvi wa mali na vifo.

"Kila mmoja wetu bila kujali uwezo wake aangalie wajane ,yatima na wazee , viongozi wa serikali wasimame na kuwatetea wenye mahitaji kwa kuwa bwana ametuagiza hivyo"

Akiwataka wote waliodhulumu wajane na Yatima kuomba Toba na kuacha tabia hiyo kwani wanaweza kulaaniwa.

"Wajane na yatima wamekuwa wakinyimwa haki ndani ya familia na nje ya familia,wananyang'anywa mali,wanadhulumiwa haki zao walizochuma na wenza wao kama nyumba ,viwanja ,watoto na pesa zilizopo benki, tukitaka baraka lazima tuyajali makundi haya vinginevyo tutalaaniwa" 

Naye mwalimu wa watoto yatima wanaofadhiliwa na kanisa hilo Nazareth  Laizer alisema utaratibu wa kanisa la Naivera wa kuyakumbuka makundi maalumu na kula nao chakula , umejenga faraja na kuwafanya wajisikie hawako peke yao bali mtetezi wao yu hai.

Aliwataka watu wengine kuiga mfano huo ili kuwasaidia watu wasio na uwezo na kuwatia faraja ili wajisikie hawapo peke yao.

Ends...


Post a Comment

0 Comments