FULL STORY KIGOGO WA POLISI ARUSHA ADAIWA KUKODI MAJAMBAZI KUMUUA MUMEWE,TIZAMA PICHA ATIWA MBARONI, YUMO HAWARA YAKE

  By Ngilisho Tv Arusha


Jeshi la Polisi Mkoa wa
Arusha linamshikilia mkaguzi msaidizi wa polisi kituo cha USA River , Demetrida Sweethbert Thadeo akidaiwa kukodi majambazi ili kumuua mumewe,Daudi Thomas Ayo kutokana na ugomvi wa kifamilia uliokuwa ukiendelea ndani ya wawili hao.

Taarifa za uhakika zimedai kwamba Demetrida alikamatwa kwa tuhuma hizo  na tayari baadhi ya watuhumiwa wa tukio hilo wanashikilika na miongoni mwa majambazi wanaohusishwa na mpango huo yumo mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Ombeni anayedaiwa kuwa ni hawara wa askari huyo .

Taarifa zimedai kwamba tayari namba ya askari huyo imenyofolewa na kutumwa makao makuu ya jeshi hilo kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu.
Mume Daudi Thomas Ayo 
Demetrida Sweethbert Thadeo 

Demetrida Mkazi wa Momela wilaya ya Arumeru, anatuhumiwa kukodi majambazi waliomjeruhi kwa mapanga mumewe Daud Thomasi Ayo kutokana na ugomvi wa kifamilia wakati akijaribu kufungua geti ili aingie nyumbani kwake usiku.

Taarifa zimedai kwamba Daudi amekuwa akimtuhumu mkewe huyo kwa usaliti wa ndoa na mahusiano ya kimapenzi yasiyofaa.
Jambo linaloweza kuchangiwa na hawara kushiriki njama za kumuua ili wawe huru na mahusiano.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani za jeshi hilo na kuthibitishwa na Mumewe, tukio hilo lilitokea usiku wa Desemba 24, 2023 nyumbani kwao Momela ambapo watu wasiojulikana walimvamia akiwa anaingia nyumbani kwake akijaribu kufungua geti ndipo watu wanne wakiwa na mapanga walijitokeza na kuanza kumkatakata  sehemu mbalimbali za mwili wake.

"Kwakweli Daudi alijeruhiwa sehemu za kichwani na sehemu ya shingo na alikatwa vidole vitatu vya kiganja, inaonekana walitaka kumchinja ila wakati wakiendelea kumkata alianguka chini ndipo walipoona wamemaliza kazi na kutoweka "kilisema chanzo

Inadaiwa kuwa siku chache kabla ya tukio hilo Demetrida alionekana akiharibu mfumo wa kamera za nyumbani kwao (CCTV Camera)na mumewe alipomuuliza kwanini anazima kamera hakuweza kutoa majibu ya maana ila alisema anarekebisha.

Taarifa zinasema kuwa wanandoa hao ambao wamebahatika kuwa na watoto wawili akiwemo mdogo wa kunyonya wa miezi minne, Mume amekuwa akimtuhumu kujihusisha na mahusiano yasiofaa na mara nyingi tangia amejifungua alikuwa hamnyonyeshi mtoto ipasavyo na wakati mwingine amekuwa akilala nje ya ndoa na kurejea asubuhi au baada ya siku kadhaa.

Ayo ambaye hufanya kazi  katika kampuni ya udalali wa mashamba ya Kambele, alilazwa katika hospitali ya ALMC(Selian), jijini Arusha, alithibitisha kuvamiwa na majambazi  ila aligoma kuzungumzia kwa undani tukio hilo.

Hata hivyo kati ya watu wanne waliomvamia siku hiyo mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Agustino anashikiliwa katika kituo hicho cha polisi na upelelezi unaendelea.

Taarifa zimedai kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi, alikiri kuhusika na tukio hilo na kueleza kuwa yeye na wenzake walitoka Dar es salaam baada ya kuahidiwa na askari huyo ujira wa sh. milioni 3 na tayari walikabidhiwa kitita cha sh. 400,000 kama malipo ya awali kwa ajili ya kumuua mumewe.

"Hawa vijana aliwakodi kutoka Dar ili wamuue mume wake na miongoni mwa watuhumiwa hao mmoja ni hawara yake anaishi hapa Arusha na siku ya tukio  mkewe (Askari) alikuwemo ndani ila alizima CCTV CAMERA na mumewe alipokuja majira ya saa nne usiku vijana hao walimvamia baada ya kuteremka kwenye gari na kuanza kumkatakata na alipoanguka chini walijua amekufa na wote walitoweka" kilisema chanzo 

Daudi alipotakiwa kuongelea tukio hilo mara ya kwanza alikubali na kuahidi kutoa ushirikiano lakini baadaye alipoitwa kutoa maelezo kituo cha polisi aliomba asiongee na mwandishi wa habari kwa madai kwamba amekatazwa na polisi kwa madai ataharibu uchunguzi.

Baadhi ya askari polisi kituoni hapo wamesikitishwa na tukio hilo wakidai kwamba mara kadhaa mumewe amekuwa akija kituoni hapo kwa mkuu wa kituo afande ODC, kulalamika kuhusu tabia na mwenendo wa mkewe.

Baba mzazi wa Daudi, Thomas Ayo alikiri kuwa ndoa ya wawili hao ina mgogoro wa mara kwa mara na amesikitishwa sana na tukio hilo.
Mzee Thomas Ayo 
Nyumbani kwa Daudi na Mkewe 
"Tarehe 26 mwezi 12/2023 mke wake na Daud alinipigia simu akaniambia mme wake amekatwakatwa na majambazi "

"Hivi sasa Daud ambaye ni MTOTO wangu amechanganyikiwa amekuwa kama kichaa hawezi kuongea kitu kinachoeleweka ndio maana Mimi nimejitokeza kuongea na waandishi wa habari ,ila Mimi Nilikuwa nikiamua ugomvi wao mara kwa mara na huyo mke wake aliwahi kunitamkia kuwa mtoto wako ananitesa na mimi nimetoka kamda ya ziwa sitakubali ipo siku itafika mwisho , mmoja lazima ataenda kaburini na mwingine magereza"

Aliiomba serikali isaidie ichukie hatua za kisheria "naona hili jambo linapoapoa" 

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alipoulizwa alisema bado hajapata taarifa ila aliahidi kulifuatilia kwa wasaidizi wake na kulitolea ufafanuzi.

"Ndo nalisikia kwako ila ngoja nifuatilie nitakupa taarifa"

Hata hivyo ndugu na jamaa wamelalamikia hatua ya askari huyo kutochukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi kwani kwa kuwa anakabiliwa na tuhuma nyingi ambazo jeshi hilo linazifumbia macho.

Ends......

Post a Comment

0 Comments