Na Joseph Ngilisho- Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linamshikilia dereva bodaboda, Amedius Mfoi (25) mkazi wa Muriet Jijini Arusha kwa tuhuma za kumuua kwa mchinja mtoto wake , Amani Amedius Mfoi (3).
Mtoto Amedius Mfoi enzi za uhai wakeAkitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha , Justine Masejo alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 23,2024 muda wa saa 12:00 jioni katika mtaa wa Murieti , manisipaa ya jiji la Arusha.
Kamanda Masejo amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alimkata shingo mtoto huyo na kitu chenye ncha kali na kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kicha vipande vya mwili ikiwemo kichwa kuviweka kwenye ndo ya maji na kufunika.
Aidha ameeleza kuwa baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi mara moja Jeshi hilo lilianza uchunguzi na kumtafuta mthumiwa huyo kwa kushirikiana na wananchi ambapo walifanikiwa kumkamata muda mchache baadae.
ACP Masejo amesema baada ya uchunguzi Jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
Akizungumzia tukio hilo babu wa marehemu Mzee Isack Mfoyi alisema kuwa kuanzia mchana alikuwa anamtafuta mjukuu wake ambapo siyo kawaida yake kutoonekana nyumbani.
Alisema majira ya saa kumi na mbili jioni akiwa nyumbani alisikia harufu ya makande kuungua jikoni ndipo alipoenda kuchukua ndoo ya maji lakini alipofunua ndo ya maji alikuta kichwa cha mjukuu wake huku mwili ukiwa kwenye ndoo nyingine imefunikwa.
Hata hivyo hadi sasa haijafahamika chanzo cha mtuhumiwa kutenda tukio hilo.
Ends..
0 Comments