DC ATANGAZA MSAKO WA DUKA KWA DUKA KWA WALANGUZI WA SUKARI ARUSHA ,UKIUZA ZAIDI YA 3000 KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAKUHUSU,MKURUGENZI ALPHA GROUP AFUNGUA MILANGO YA REJAREJA NI SH,3000 TU KWA KILO,UKIUZA ZAIDI YA 3000 KIBANO KIKALI KINAKUHUSU ,WATENDAJI WA MITAA NA KATA WAPEWA MENO KUONGOZA MSAKO

Na Joseph Ngilisho, Arusha 


Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtehengerwa ameahidi kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwafikisha mahakamani, wafanyabiashara wanaouza sukari kwa bei ya juu tofauti na maelekezo ya serikali na kuagiza vyombo vya dola watendaji wa mitaa na kata  kufanya msako wa duka kwa duka.


Mtehengerwa ameyasema hayo wakati alipofanya ziara  ya kushtukiza kwa wakala mkubwa wa Sukari mkoani hapa, kampuni ya Alpha Group LTD, na kumpongeza mfanyabiashara huyo kwa  uzalendo aliouonesha wa kutii maelekezo ya serikali kwa kuuza sukari kwa bei ya shilingi 3000 kwa rejareja na shilingi 2800 kwa wanunuzi wa jumla.

Katika jiji la Arusha sukari imekuwa ikiuzwa kati ya shilingi 3500 hadi 5000 na upatikanaji wake ni shida ,jambo ambalo limewafanya wananchi walalamike ikiwemo baadhi ya vyakula kupanda mahotelini.


Mkuu huyo wa wilaya ambaye aliambatana na kamati yake ya ulinzi na usalama, aliwaagiza viongozi wa mitaa,watendaji na makatibu kata na Tarafa kufanya masako katika maeneo yao na kuwakamata wafanyabiashara watakaobainika kuuza sukari kinyume na bei iliyotolewa na serikali  ya sh,3000 .

"Kuanzia sasa Mfanyabiashara atakayebainika kuuza sukari kinyume na bei ya sh,3000 atakamatwa na tutamfungulia kesi ya uhujumu uchumi ,hatuwezi kukubali wananchi wapate shida wakati serikali yao ipo na kuanzia leo tumetoa maelekezo kwa viongozi wote wa mitaa, kata na tarafa wafanye msako Duka kwa duka na kuwakamata wale wote wanaouza sukari kinyume na maelekezo ya serikali"


Mtehengerwa aliwahakikishia wananchi kwamba jiji la Arusha bado lina sukari ya kutosha huku kampuni ya Alpha Group pekee ikiwa na akiba ya tani 307 katika kipindi hiki ambacho viwanda vimepunguza uzalishaji sababu ya mvua ila alisema kuna wafanyabiashara wanatumia fursa hiyo kujinufaisha kwa kuficha sukari ili wauze kwa bei ya juu ambapo amejipanga kuwachukukia hatua.






Aliwataka wananchi kuacha kulalamika wakiwa wametulia bali watoe taarifa kwa viongozi au wapige simu kwake kupitia namba yake  ya simu 0767 140136 pindi watakapobaini kuna wafanyabiashara wanauza sukari kwa bei ya juu.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Alpha Group LTD  inayojihusisha na uwakala wa kusambaza bidhaa mbalimbali  ikiwemo sukari,Karim Dakik alisema kumekuwepo na uhaba wa sukari inayotokana na viwanda kupunguza uzalishaji ila aliswma kampuni yake imekuwa ikiagiza kutoka viwanda mbalimbali nankuwauzia wananchi kwa bei elekezi ya shilingi 3000.


Alisema wanaunga mkono bei elekezi ya serikali ya shilingi 3000 na ameamua kufungua duka la rejereha ili kuwahudumia wananchi kwa bei ya shilingi 3000 na kuwataka wasiogope kuja kununua sukari kwake ili kupata unafuu wa maisha.


"Tuna changamoto kidogo ya sukari lakini tunaunga mkono bei elekezi ya serikali ya shilingi 3000 ndio maana tumefungua Duka la rejareja ili kuwapatia unafuu wananchi ,kwa sasa tunatani 307 zitakazotoshea kwa muda ila tunaendelea kuagiza sukari maeneo tofauti ili tuwauzie wananchi kwa bei nafuu"


Alisema viwanda vingi vya sukari hapa nchini vimepunguza uzalishaji kwa sabahu ya mvua, miwa imejaa maji na kupunguza utamu ,hivyo wanajitahidi kukabilia na hali hiyo kuhakikisha wananchi wanapata sukari kwa bei nafuu.



Ends....







Post a Comment

0 Comments