ASKARI POLISI (TRAFFIC) MAARUFU ARUSHA, AKAMATWA AKISAFIRISHA SHEHENA YA DAWA ZA KULEVYA,TAZAMA PICHA ZA TUKIO NDANI

Na Joseph Ngilisho MANYARA 

Jeshi la Polisi Mkoani Manyara linamshikilia askari wa Usalama Barabarani Mkoani Arusha,  SGT Ismael Katenya(48)kwa kosa la kusafirisha shahena ya dawa za kulevya aina ya mirungi mabunda 340 yenye uzito wa kilo 140 yakiwa kwenye mabegi.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi Mkoani humo,askari huyo mwenye namba F.3544 alikamatwa jana majira ya tisa alasiri katika kijiji cha Silaloda wilaya ya Mbulu Mkoani humo akitumia gari lake aina ya Nissan Patrol, kusafirisha biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wenzake wakiokuwa doria akisafirisha dawa hizo akiwa na gari lenye namba 148 CTB aina ya Nissan Patrol Steshen Wagon rangi Nyeusi linalodaiwa ni mali yake.


Taarifa imedai kuwa askari hao walilitilia shaka gari hilo na  baada ya kulisimamisha  na kufanya upekuzi,ndipo walipobaini kuwepo kwa vifurushi vitano vya gunia na mabegi mawili na baada ya kuyafungua ndipo walipokuta dawa za kulevya aina ya Mirungi. 


Taarifa ilifafanua kwamba askari hao wakiongozwa na OC CID wilaya ya Mbulu A.Mweluvimbo walipekua shehena hiyo na kukuta vifurushi hivyo vimefungwa   mifuko miwili ya Salfeti ikiwa na bunda kati ya 40 na 50 na kwenye mabegi mawili kuna mabunda  85 Na 53.


Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi Mkoani humo,RPC George Katabazi alithibitisha kukamatwa kwa askari huyo na kueleza kuwa anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi  ili kubaini wahusika halisi wa mtandao wa biashara hiyo haramu.

RPC Katabazi 

Alisema chanzo cha askari huyo kufanya biashara hiyo ya kusafirisha 

Mihadarati ni kujipatia kipato kwa njia haramu jambo ambalo alidai kuwa ni kunyume cha sheria kwa mtu yoyote hususa mtuhumiwa ambaye ni mtumishi wa serikali.

"Tumemkamata akiwa peke yake katika doria zetu za kawaida na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na utakapokamilika tutamfikisha mahakamani"alisema Katabazi

Kamanda katabazi alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.


Ends....



Post a Comment

0 Comments