Na Joseph Ngilisho Arusha
Viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Arusha,Lokeni Masawe,Mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya, Dominic Mollel na mwenyekiti wa maduka ya standi ndogo ,Lorandi Kwayu ,walipigiwa simu ya wito kwenda kituo cha polisi wakati wakiongoza mkutano wa wafanyabiashara waliojikusanya eneo hilo la standi ndogo kujadili sakata hilo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao wilaya ya Arusha Dominic Mollel,alikiri kuitwa kituo cha polisi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa 3 juu ya mikataba ya ujenzi wa vibanda hivyo na baadaye walidhaminiwa.
"Mimi na mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa Loken Masawe na mwenyekiti wa maduka standi ndogo wote tuliitwa polisi na kushikiliwa kwa masaa kadhaa tukihojiwa kuhusu mikataba ya ujenzi wa vibanda vya biashara"alisema Mollel
Hivi karibuni mkurugenzi wa jiji hilo,Mhandisi Juma Hamsini alitishia kuvipiga mnada vibanda vya wafanyabiashara hao kwa watu wengine iwapo wafanyabiashara hao wajenzi wanaendelea kukaidi kujisajili mikataba mipya yenye ongezeko la pango kutoka sh,laki 2 hadi laki mbili na nusu.
Wafanyabiashara hao wamegomea utaratibu wa Mkurugenzi huyo, wakiwa na madai kwamba wao ni wajenzi na wanapaswa kutambulika kama wamiliki halali wa vibanda na sio wapangaji, hivyo hawapaswi kujisajili kama wapangaji kupitia mfumo mpya wa ukusanyaji mapato ya serikali wa TAUSI.
Akiongea katika mkutano huo katibu wa wafanyabiashara hao Angelus Shokia alimwomba waziri Mkuu Majaliwa Kasimu Majaliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro huo ambao unadalili mbaya za kufifisha mapato ya serikali.
Alisema halmashauri ya jiji la Arusha imekuwa ikikusanya mapato kutoka vyanzo hivyo zaidi ya sh,milioni 900 kwa mwaka na wanashangaa jiji kutaka kuwapoka vibanda hivyo baada ya kuingiwa na tamaa kuwa wajenzi wanafaidi zaidi.
Alisema kuwa mgogoro huo umekuwa ukiibuka mara kwa mara hasa kunapokaribia uchaguzi na waziri mkuu Majaliwa aliwahi kuingilia kati na kuzuia utoaji wa mikataba mipya na kubariki wafanyabiashara hao kuendelea kumiliki vibanda hivyo kama wajenzi bila kubughudhiwa.
"Hili jambo limekuwa likijirudia mara kwa mara mwaka 2016 waziri Mkuu Majaliwa aliingilia kati na kutoa maelekezo kupitia barua aliyoitoa desemba 3, 2016 na nakala kupelekwa kwa Mkurugenzi jiji la Arusha na kwa katibu tawala mkoa wa Arusha"
Shokia alisema katika miaka tofauti ya 1990 wafanyabiashara hao waliingia makubaliano na halmashauri hiyo kujenga maduka hayo huku halmashauri ikimiliki Ardhi na wao walimiliki maduka hayo kwa muda usio na kikomo.
Shokia akilalamika hatua ya wao kuitwa vishoka,madalali au mpangaji wakati mikataba yao ya mwanzo inawatambua kama wajenzi na haujawahi kubadilishwa .
"Sisi hapa hatuachii na hatuondoki atakayekuja kutuondoa hapa ni rais Samia au Waziri Mkuu Majaliwa na tunawaomba waingilie kati jambo hili tumechoka kunyanyaswa kila siku tubafuatqa na askari wwnye bunduki utazani sisi ni majambazi"
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Arusha mhandisi Juma Hamsini aliwataka wafanyabiashara hao kufuata utaratibu wa serikali ikiwemo kujaza fomu za mikataba mipya nankujisajili kupitia mfumo wa TAUSI .
Alisema katika zoezi la siku mbili walizoweka kambi eneo hilo la standi ndogo wafanyabiashara zaidi ya 65 wameshajisajili kupitia mfumo wa TAUSI na kudai kuwa kikundi cha watu wachache wakiongozwa na viongozi hao ndio wanasumbua kwa kuwahadaa wengine kugomea mfumo huo.
Alisema kwa sasa ameanzisha mobile Court ambapo kwa wale wasiozingatia taratibu kibiashara kwa kuhujumu mapato ya serikali, watapewa wito wa mahakama au watafuatwa nyumbani na mahakama inayotembea pamoja na gari la mahabusu .
Ends..
0 Comments