TAZAMA PICHA MAZISHI YA BABA WA BILIONEA MSUYA YALIVYOTIKISA MERERANI, WATU WAFURIKA WAPOTEZANA, BARABARA YAFUNGWA, AZIKWA KARIBU NA KABURI LA MTOTO WAKE BILIONEA MSUYA,FAMILIA YAMLILIA

Na Joseph Ngilisho, ARUSHA


Mamia ya wakazi wa Mji wa Mererani, wafanyabiashara ndugu na jamaa wamefurika kumzika baba wa marehemu Bilionea Msuya,Mzee Simoni Msuya(80) aliyezikwa jana nyumbani kwake Cairo Mererani, Mkoani MANYARA. 


Katika Mazishi hayo  Barabara ilifungwa kwa masaa kadhaa Kutokana na wingi wa watu  ili Barabara hiyo kutumika kwa ajili ya maegesho huku wananchi wa Mererani wakisimamisha shughuli za kiuchumi kumsindikiza mpambanaji Mzee Msuya. 

Jirani na mnara wa kaburi la kifahari la mtoto wake Bilionea Msuya, mwili wa marehemu Msuya ulilazwa na vilio vilitawala kiasi cha watu kuzimia wakati jeneza la thamani likiteremshwa kwa upole ndani ya nyumba yake ya milele. 

Marehemu Msuya alifariki Novemba 30 mwaka huu jijini Dar Es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi yaliyomsibu na kuzikwa nyumbani kwake huku msiba huo  ukitawaliwa na vilio kutoka kwa ndugu wenye uchungu na marehemu Msuya. 

Akiongoza ibada ya mazishi iliyokuwa imefurika mamia ya waombolezaji,Mch Zakayo Palangyo Mkuu wa jimbo kusini kutoka  Dayosisi ya Meru, alimweleza marehemu kuwa ni nguzo muhimu iliyoanguka ikiwa inahitajika .

Mch Palangyo alisema kuwa marehemu Msuya alikuwa mpambanaji asiyechoka na kamwe hakuwahi kuchoka katika maisha yake ya utafutaji hasa katika sekta ya madini na ndio chimbuka la utajiri wa marehemu mtoto wake Erasto Msuya. 

Aliwasihi familia ya marehemu kuyaishi na kuyaenzi yale mema ya marehemu Msuya kwani hayupo mbadala wake na kuiomba familia hiyo akiwemo mjane Ndeshikurwa Msuya kuilinda vizuri kamilia hiyo aliyoachwa na marehemu katika mikono yake salama .


Akisoma risala fupi ya Marehehemu Mmoja ya watoto wa Mzee Msuya alisema baba yake alifariki Novemba 30 mwaka huu, wakati akipigania uhai wa Maisha yake katika hospitali binafsi jijini Dar es salaam. 

Watoto watano kati ya Saba wa Marehemu Msuya panoja na mama Yao kwa sasa ni Mjame Ndeshukurwa Msuya walimpigania apone na arejee kuendeleza familia yake lakini haikuwa hivyo Bali mungu alimpenda zaidi. 

Mzee Msuya alizaliwa January 2,1943 katika kijiji cha Shingatini ,Usangi Mkoani Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa nne Kati ya watoto nane . 

Ameacha Mjane na watoto watano, wajukuu 22 na vitukuu 6 . Pia ameacha utajiri wa Mali kibao yakiwemo Mashamba, Migodi, Magari, Majumba na Fedha. 





















Ends







Post a Comment

0 Comments