SILINDE ATAKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU ZITUMIE TAFITI KUISAIDIA JAMII,AKIPONGEZA CHUO CHA UHASIBU(IAA) ARUSHA,MKUU WA CHUO APIGA BAO AFIKISHA KOZI 71 WAHITIMU KIBAO WAONGEZEKA

 Na Joseph Ngilisho Arusha 

Naibu waziri wa kilimo, David Silinde amezitaka Taasisi  za elimu ya juu kuisaidia jamii kwa kufanya tafiti na kutumia matokeo ya tafiti hizo katika kuanzisha mitaala inayoakisi mazingira halisi ya watanzania.


Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipohudhulia mahafali ya 25 ya chuo cha uhasibu Arusha(IAA) ,yaliyofanyika katika hoteli  ya kitalii ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha, ambapo jumla ya wahitimu 5000 walimaliza masomo yao na kutunukiwa Astashahada, Stashahada, shahada na shahada ya Uzamili ya chuo cha uhasibu Arusha katika fani mbalimbali walizosoma.
 

Naibu waziri alisisitiza kuwa iwapo tafiti hizo zikifanywa kwa weledi na umahili ,wahitimu watakaoandaliwa kupitia mitaala hiyo watakuwa na uwezo wa kutumia elimu na maarifa walioyapata kutatua changamoto za watanzania na kusaidia kukuza uchumi wa taifa.

"Moja ya malengo ya millenia ifikapo mwaka 2030 ni kuhakikisha elimu bora na yenye usawa kwa wote inatolewa Kote ulimwenguni"



Said Mtanda Mhitimu IAA-2023 

David Kileo Mhitimu IAA-2023

Saipulani Ramsey Mhitimu IAA-2023

Alikipongeza chuo hicho cha uhasibu Arusha kwa kujiwekea malengo ya pekee ya kuzalisha wataalamu mahiri ,wenye weledi wanaosifika na kukubalika sokoni kutokana namna wanavyooandaliwa.

Aidha alitoa rai kwa wahitimu kutumia matokeo ya tafiti walizofanya kutatua changamoto za jamii kwa kuzishirikisha kuliko kuzifungia.

Awali mkuu wa chuo hicho,Prof Eliamani Sedoyeka alisema katika mwaka wa fedha 2023/24 chuo kimefanikiwa kuanzisha kozi mpya nne,tatu zikiwa za shahada na moja shahada ya uzamili ambazo ni shahada ya Media Anuwai na mawasiliano kwa umma,shahada ya uhasibu wa fedha ,shahada ya usimamizi wa nyaraka na taarifa na shahada ya uzamili katika usimamizi wa elimu.

Alisema kuanzishwa kwa kozi hizo ,chuo hicho kimefanya kiwe na jumla ya kozi 71 ambapo kati ya hizo ,kozi 17 za Astashahada,kozi 24 ni shahada na kozi 14 ni shahada ya uzamili. 

Aidha alisema IAA ipo katika hatua ya uhuishaji wa mitaala iliyopo chini ya mradi wa elimu ya juu  kwa mageuzi ya kiuchumi(HEET) ikiwa lengo ni kuboresha mazingira ya soko la ajira kupitia wataalamu wa chuo hicho kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya umma na binafsi.

Alisema mpango na malengo ya chuo mwaka 2022/23 hadi mwaka 2026/27 ni kuongeza wigo wa kutoa elimu kitaifa na kimataifa hususani katika nchi za EAC na SADC kupitia kampasi zake nne zilizopo  Arusha,Babati,Dar es salaam na Dodoma .

 

"Kuanzia mwaka 2024 tunatarajia kuanza kujenga kampasi mpya ya Songea Mkoani Ruvuma"

Naye Mwenyekiti wa baraza la Uongozi IAA,dkt Mwamini Tulli ambaye taarifa yake ilisomwa  na Joseph Mwigune, alisema atahakikisha malengo,mikakati na mipango ya chuo ya kutoa mafunzo na tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu yanatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Alisema katika mwaka huu wa masomo  2023 jumla ya wahitimu walikuwa 5000 kutoka matawi ya chuo cha Arusha,Babati na Dar es salaamikilinganishwa na mwaka jana 2022 walikuwa wahitimu 3529 na lengo la chuo ni kuwa kitovu cha ubora katika utoaji wa mafunzo na kuandaa wataalamu wa fani mbalimbali wenye ujuzi na weledi wa hali ya juu.

Kwa upande wa baadhi ya wahitimu wa chuo cha IAA,Said Mtanda Mkuu wa Mkoa wa Mara na Davidi Kileo walitoa rai kwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali nchini kutopweteka na elimu walionayo bali wajijengee tabia ya kujiendeleza kimasomo kwa lengo la kutatua changamoto za wananchi kwani  dunia ya sasa ni ya teknolojia na utandawazi.

"Mimi hapa ni mkuu wa mkoa nina Masters sitafuti kazi ninaajira tayari, Sikuja kusoma hapa kutafuta cheti kama kazi ninayo,wito wangu kwa vijana tusilete ujanja ujanja kwenye elimu twende tutafute ujuzi zaidi tusaidie wananchi wetu"

Naye Saipulani Ramsey Katibu wa siasa na uenezi( ccm) Mkoa wa Arusha,mhitimu wa shahada ya uzamili wa sayansi ya mipango na usimamizi wa miradi alisema tafiti walizofanya katika kipindi chote cha masomo zitumike kutatua shida na changamoto za wananchi .

Alitoa rai kwa wahitimu kuitumia elimu walioipata kuleta mabadiliko chanya yenye kuakisi changamoto za watanzania na kuleta ajira kwa vijana.

Ends....







Ends.....






Post a Comment

0 Comments