SHIRIKA LAKERWA NA MAAMUZI YA HAKIMU ALIYEMWACHIA HURU BABA ALIYEMLAWITI MTOTO WAKE MBELE YA MAMA YAKE ,NI BAADA YA KUMFUKUZA MAMA KITANDANI,LAMLILIA WAZIRI GWAJIMA KUINGILIA KATI

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Shirika linalojihusisha na utetezi wa haki ya wanawake na watoto Mkoa wa Arusha la Mimutie women organization limesikitishwa na mwenendo wa uendeshaji wa kesi ya mtoto aliyebakwa na kulawitiwa na baba yake mzazi kwa kuendeshwa kinyemela na kisha mtuhumiwa kuachiwa huru.


Akiongea kwa uchungu Mkurugenzi wa Shirika hilo,Rose Njilo alisema hali hii inakatisha tamaa jitihada za serikali na wadau wa masuala ya ukatili kukomesha ukatili dhidi ya watoto hapa nchini.
Rose Njilo Mkurugenzi ,Mimutie

Alisema alipata taarifa juu ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10,mwanafunzi wa darasa la Tano wa shule ya Msingi Terath jijini Arusha(jina limehifadhiwa) kulawitiwa na baba yake mzazi mara kwa mara chumbani usiku.

Alisema kutokana na uwezo mdogo wa kipato kwa familia  ya mtoto mwathirika ,aliamua kuwawezesha Nauri mama wa mtoto huyo ili suala hilo aweze kulifikisha kwenye vyombo vya dola ikiwemo mahakamani.

Alisema mara baada ya mtuhumiwa anayetambulika kwa jina la Hassan Shemhilu mkazi wa mtaa wa Nyangulo, Murieth jijini Arusha,kukamatwa na kufikishwa mahakamani hakuridhishwa na mwenendo wa shauri hilo namba 32/2023,  liliyokuwa ikiendesha na mahakama ya wilaya mbele ya hakimu Mkazi Bitony Mwakisu aliyemwachia huru mshtakiwa huyo.

"Kwakweli hii kesi imenisikitisha sana tangia ianze kusililizwa February mwaka huu imekuwa na kizungumkuti tangia ukamataji wa mtuhumiwa hadi uendeshaji wa shauri hilo mahakamani haukuwa wazi".

"Nakumbuka tulipokuwa tunaenda mahakamani nashangaa tunaambiwa kaeni hapa msubiri kesi kuitwa ,lakini chaajabu tukiwa hapo na muusika tunasubiri kuitwa unaona watu wakitoka chumba cha mahakama ukiuliza unaambiwa kesi imeahirishwa, kwakweli mimi kama mtetezi wa watoto sijaridhika na namna kesi hii ilivyoendeshwa kiukweli nilikosa ushirikiano ikiwemo kwa wakili wa serikali, Belinda Rwakatale aliyekuwa akiendesha shauri hilo "

Rose alisema kesi hiyo ilitolewa uamuzi Novemba 24 mwaka huu kwa kumwachia huru mshitakiwa pamoja na ushahidi wa mtoto na mzazi lakini hakimu hakuona kosa la kumtia hatiani mshtakiwa na kuamua kumwachia huru.

"Kilichofanyika hapa ni hujuma nyingi mtoto amekosa haki yake na amezidi kusononeka ,nikimhoji wakili wa serikali imekuwaje maamuzi yamekuwa hivyo wakati kulikuwa na ushahidi wa uhakika ukiwemo wa daktari alinijibu kuwa mshtakiwa naye alipewa haki ya kusikilizwa 

Rose alimwomba waziri mwenye dhamana Dorothy Gwajima kuingilia kati na kufuatilia suala hilo ili kuona wapi haki ya mtoto ilipopindishwa na kuchukua hatua kwa lengo la kukomesha matukio ya aina hiyo.

Naye mama wa mtoto huyo,Faudhia kaimba alisema aligundua mtoto wake kulawitiwa baada ya  kumwona  akimfuata kitandani baba yake  usiku na kuanza kumwingilia. 
Faudhia Kaimba,Mama wa Mtoto aliyelawitiwa na baba yake
"Nilipomhoji mtoto aliniambia baba yake amekuwa akimfanyia hivyo mara kwa mara hasa ninapokuwa nimeenda kutembeza biashara zangu mjini

Alisema alitofautiana na mume wake akamfukuza kitandani akawa analala chini , lakini siku moja majira ya saa 9 usiku alimwona  mtoto wake akimfuata baba yake kitandani.
" Niliingiwa na hofu nilisubiri kukuche na ilipofika asuburi nilimwita na kumhoji ndipo aliponiambia kuwa baba yake huwa anamfanyia kitendo kibaya kwa kumbaka mbele na nyuma na kumwingizia vidole

Baada ya kupata taarifa hiyo aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi cha kati mjini Arusha na mtoto alifanyiwa vipimo na kughundulika kuwa mtoto ameharibiwa sehemu zote za siri.

Alisema kesi hiyo ilienda mahakamani ambapo yeye na mtoto walitoa ushahidi lakini baadaye wakawa wanazuiwa kwenda kusikiliza ikiwemo kutopewa uwazi kinachoendelea na baadaye walipata taarifa kuwa hukumu ya kesi hiyo imetolewa na mtuhumiwa ameachiwa huru.

Kwa Upande wa Mwathiriwa wa tukio hilo,Mwanamkasi Jumaa(sio jina lake)alisema kuwa baba yake alianza kwa mara ya kwanza kumbaka baada ya kumwita na kumshika maziwa baadaye alianza kumfanyia kitu kibaya huku akimtishia kuwa iwapo atasema atamkata masikio.

Mtoto mwathiriwa na ukatili wa baba yake
"Siku moja nikiwa nimelala mama aliniona nikipanda kitandani kwa baba yangu aliyekuwa ameniita, aliniuliza naenda kufanya nini, sikumjibu kitu, akaniambia nirudi kulala ninapolala na asubuhi nitamweleza vizuri

Alisema baba yake alikuwa akimbaka mara kwa mara USIKU  wakati mama yake akiwa amelala chini baada ya kumfukuza kitandani au wakati mama akiwa ameenda mjini kufanyabiashara ya kutembeza bidhaa zake

Ends...













Post a Comment

0 Comments