Na Gift Mongi
Moshi
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amemshukuru rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa utayari wake katika kupeleka maendeleo kwenye jimbo hilo.
Prof Ndakidemi amesema hadi kufikia mwezi julai tayari fedha kiasi cha bilioni 35.1 zilikuwa zimefika katika jimbo hilo kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kimandeleo na kupunguza kadhia iliyokuwa ikiwakumba wakazi wake
'Nimshukuru rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake wa pekee katika jimbo la Moshi Vijijini kwa fedha tulizozipata'amesema
Kwa mujibu wa Prof Ndakidemi ni kuwa kiwango hicho cha fedha ni sawa na kile kilichopelekwa katika jimbo la Vunjo linalowakilishwa na Dkt Charles Kimei
Aidha Prof Ndakidemi amesema kiasi hicho cha fedha kimeenda katika miradi mbalimbali ya kimandeleo kama vile afya,maji, barabara,na mambo mengineyo.
Prof Ndakidemi anatoa pongezi hizi mbele ya waziri wa tawala za serikali za mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa akiwa mgeni rasmi katika hafla ya uwasilishwaji wa ilani ya uchaguzi 2020-2025.
Kwa mujibu wa Prof Ndakidemi ni kuwa fedha hizo zimegusa maisha ya wananchi moja kwa moja na kuwa lazima usimamizi uliofanyika upongezwe
'Naomba niwashikuru viongozi wangu wa chama katika usimamizi huu mzuri wa miradi ya kimandeleo na hata hizi fedha ninazozisema hata huku Vunjo zimekuja'amesema
Erasmus Mallya mkazi wa kata ya Okaoni jimbo la Moshi Vijijini amesema kuwa ipo miradi mbalimbali inayokelezwa na kuwa italeta tija kwa wananchi walio wengi.
'Tulishindwa kwa kipindi kirefu ila sasa mama(Dkt Samia Suluhu Hassan)kahamua unaona mambo yanavyokimbia'anasema
Mwisho...
0 Comments