OLAIS LUKUMAY CHIPUKIZI ALIYEWABWAGA WENZAKE BILA HURUMA ,NIMWAKILISHI PEKEE WA MKUTANO MKUU WA CHIPUKIZI CCM TAIFA ARUMERU

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Kijana chipukizi wa CCM, Olais Johannes Lukumay ameibuka mshindi wa nafasi ya  uwakilishi wa mkutano mkuu wa chipukizi Taifa akitokea wilaya ua Arumeru Mkoa wa Arusha baada ya kuwabwaga kwambali washindani wake.


Awali wagombea wapatao sita walichuana vikali ambapo Lukumay alipata kura 14 na kufuatiwa na Alina Lungaisa aliyepata kura 12,Emanuel Mshana kura (7) ,Mohamed Hekaheka kura 3,Ivan Nkyandalwe 3 na Aisha Omari Hatibu.

Kutokana na kura kukaribiana na mshindi kutofikia asilimia hamsini uchaguzi huo ulirejewa kwa mara ya pili kati ya mshindi wa kwanza Lukumay aliyepata kura 14 na mshindi wa pili Lungaisa aliyepata kura 12.


Katika duru ya pili ya uchaguzi 
Olaisi johanes lukumay alifanikiwa kuibuka mshindi kwa kura 33 dhidi ya 
Alina Rahma Lungaisa aliyeambulia kura 6 na hivyo msimamizi wa uchaguzi alimtangaza Olais LUKUMAY kuwa mshindi na mjumbe halali wa mkutano mkuu Taifa.


Olais ni mtoto wa dkt Johannes Lukumay ,mkuu wa chuo cha Afya cha  Cedha Arusha,mwenye ndoto za ubunge jimbo la Arumeru Magharibi.


Ends..


Post a Comment

0 Comments