MASHINDANO YA MICHEZO CRDB, WASHINDI WAOGELEA NOTI,ULIPO TUPO KINARA 2023,DC ATAKA YAIBUE VIPAJI ,

Na Joseph Ngilisho Arusha

Ulipo tupo Fc imefanikiwa kuibua mabingwa wa soka katika mashindano ya CRDB bank SUPA Cup awamu ya tatu yaliyomalizika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ikiwa ni mango wa crdb kuwaweka imara kiafya wafanyakazi wake.


"Ni msimu wa tatu wa mashindano hayo yanayoandaliwa na Benki ya CRDB yakilenga kujenga umoja na kuhamasisha michezo"alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki CRDB Abdulmajid Nsekela baada ya kukabidhi makombe kwa timu za ushindi


Ulipo Tupo FC  kutoka  Mwanza imepata ubingwa huo   baada ya kuifunga SDK Football Club ya Dar-es-salaam kwa magoli 2-1.


PIA kwa upande wa Netiboli Ulipo Tupo  Queens kutoka Mwanza k walifanikiwa kuifunga timu ya CRDB ya Kanda ya Kati ijulikanayo kwa jina la 'Popote Ina tiki  kutoka Dodoma kwa mabao 45 – 23 katika mchezo wa fainali zilizofanyika  uwanja huo huo. 


kwa mujibu wa Crescensia Grace Kajiru, kutoka Idara ya Rasilimali Watu ya taasisi hiyo ya fedha, alisema kulikuwa na timu 12 za mpira wa miguu na timu nane za netiboli katika michuano ya Kombe la CRDB Bank Supa iliyoanza  tangu Agosti mwaka huu ambapo ilizinduliwa  jijini Dar-Es-salaam na kufikia kilele Desemba mwaka huu kwa fainali hizo  jijini Arusha.


"Lengo Ni Kuwakutanisha Wafanyakazi pamoja, kuimarisha afya kwani mara nyingi wanakuwa wamekaa wakihudumia wateja  pia kupitia michezo hii inawalazimu kuwa na mazoezi,na inaenda kila mkoa na ni msimu wetu wa tatu 

" alisema Kajiru.


Timu bingwa  katika soka ilijinyakulia kombe medali ya dhahabu na kitita cha  Milioni 13, mshindi wa pili akipata milioni 9/- kikombe, huku washindi wa tatu akipata milioni 6.


Katika michezo ya netiboli wanawake mshindi alipata  milioni 13, mshindi wa pili milioni 8.


Michuano ya CRDB Supa Cup imefanyika ikiwa ni  msimu wa tatu mwaka huu na ilianza mwaka 2021.


Akizungumza katika mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtehengerwa ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema CRDC imeonesha njia na kutaka mashindano hayo mbalimbali ya kuwaunganisha na kuimarisha afya ,pia yatumike kuibua vipaji na baadaye kuwa na timu imara itakayoshiriki mashindano nchini.


Katika hatua nyingine Mtehengerwa aliipongeza CRDB kwa kuwekeza Matawi mengi ya benki hiyo ambayo yamewezesha wafanyabiashara kustawisha biashara zao kupitia huduma za benki hiyo.


Aliishauri benki hiyo kuendelea kuwekeza Arusha kwa kuwa kuna fursa nyingi za kibiashara zinazopelekea kukua kwa uchumi hapa nchini.


Aidha aliishauri benki hiyo kue ndeleza michezo ili kuibua vipaji kupitia vichezo ya mpira wa miguu na netball .












Ends..






Post a Comment

0 Comments