KISHINDO CHA MIAKA 14 YA AFRICANA LOUNGE NI BALAA,TAZAMA PICHA,INAVYOBAMBA ARUSHA NZIMA ,UKIINGIA KUHUDUMIWA HUTOKI WAHUDUMU WANAROHO NZURI BALAA

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Kutimiza miaka 14 ya
 kuanzishwa kwa bar maarufu jijini Arusha ya AFRICANA LOUNGE iliyopo Kaloleni , ni kielelezo Tosha cha ubora wa bar hiyo inayoungwa mkono na wateja wake wa ndani na nje ya Mkoa kutokana na huduma bora zinazotolewa kwa wahuduma wenye roho ya ukarimu.

Mkurugenzi wa AFRICANA LOUNGE,  Frederick Maimu alibainisha hayo wakati akiongea katika kumbukizi ya miaka 14 tangia kuanzishwa kwa kwake 2009.

Akizungumzia mafanikio ya AFRICANA LOUNGE alisema yametokana na wateja kukubali huduma zake na kwamba amejitahidi kuboresha mishahara ya wahudumu wake, ambapo muda wote wamekuwa na ukarimu wa kiwango cha juu kwa wateja kiasi kwamba mteja akiingia kula ama kunywa hatamani kutoka.

"Siri ya Mafanikio ya biashara ni uvumilivu na kufanyakazi kwa bidii bila kukata tamaa,kumwomba mungu na atakufikisha unapotaka,tunafuraha wateja wetu wameitikia kazi zetu ndio maana kila wakati wapo na sisi"

Alisema AFRICANA LOUNGE ni bar ya kwanza Arusha kulipa mishahara minono kwa wahudumu wwake ambao wamepelekea kuipenda kazi yao na kuwa kivutio kwa wateja.

"Mipango yetu ni kutoka hapa tulipo kwani kila siku tunaboresha huduma zetu lengo ni kufikia huduma za kimataifa kwani tunawateja wa kila aina wanaotoka mikoani kwa ajili ya shughuli za kiserikali "

Pamoja na kuipongeza serikali kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kibiashara ikiwemo  usalama,ameiomba iruhusu biashara ya bar ifanyike masaa 24, usiku na mchana ili kukuza uchumi wa taifa"

Mmoja ya viongozi wa bar hiyo,Caren Mwakatobe alisema siri ya mafanikio haya ni huduma nzuri inayotolewa kupitia wafanyakazi wake 

"Huduma zetu ni bora kuliko za wengine tuna vinywaji vya kila aina, vyakula vyote,nyama choma,supu mkia ,tuna TV kubwa za kutosha  kwa ajili ya wapenzi wa mpira na huduma zingine"












Ends...

Post a Comment

0 Comments