Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Aidha kanisa hilo pia limebatiza watoto wachanga wapatao 70 ikiwa ni ishara ya kuendelea kukua na kukubalika kwa kanisa hilo duniani.
Kwa kuonesha padri hatanii aliwataka wanandoa wa kike kushika kipaza sauti na kumtamkia mume wake akiwa amemkumbatia kwamba, atamzalia watoto bila kukoma hadi mayai ya uzazi yatakapoisha.
"Mume wangu ... nipo tayari kukuzalia hadi mayai ya uzazi yaishe"ni moja ya agano la wanandoa hao wakitamka kanisani.
Alisisitiza kwa wanandoa hao kuishi maisha mema ya kumcha mungu na kuwa na hofu ya mungu, kuwa watii kwa kila mwenza na kushirikiana kwa kila jambo.
Alisema siri ya kanisa hilo kufungisha idadi kubwa ya ndoa mara kwa mara ikitanguliwa na ndoa 53 zilizofungwa agosti mwaka huu 2023,alisema ni kutokana na ukaribu wa mapadri na waumini wake na kutaka kujua changamoto za waumini wao,uwazi wa mapato ya kanisa pamoja na kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya viongozi wao.
Naye padri wakili,Damian Ndege ambaye alishiriki kubatiza watoto ,alisema sherehe za kuzaliwa yesu kristu zimeenda sanjari na kubatiza watoto wapatao 72 ikiwa ni sehemu ya kukua kwa imani ya kanisa katoliki.
Aliwasisitiza wazazi kuwalea watoto hao katika misingi ya imani ya kikristu ili kuwaepusha na matendo maovu yasiyompendeza mungu.
𝓔𝓷𝓭𝓼𝓮
0 Comments