Na Joseph Ngilisho, Simanjiro
Kampuni ya Franone Mining and Games limetd inayojishughulisha na uchimbaji madini ya vito ( Tanzanite) imeungana na watanzania wengine na Serikali katika kuchangia mahitaji mbalimbali ya chakula Kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea wilaya ya Hanang' mkoani Manyara .
Akizungumza na waandishi wa Habari Disemba 10,2023 Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Vitus ndakize Amesema kuwa wameguswa sana na tukio hilo hivyo wao kama watanzania waliowekeza kwenye uchimbaji wa madini na wao wameona wachangie watanzania wenzao ambao wamepatwa na majanga hayo Kwa kutoa bidhaa mbalimbali.
Amesema miongoni mwa vitu ambavyo wamechangia na kukabidhi Kwa mkuu wa Wilaya Dkt. Seleman Selela ni pamoja na magunia 200 ya mahindi , maharage gunia 40 ,Sukari mifuko 20, na mafuta kantoni 40 za Lita Moja Moja ambayo imegharimu fedha za kitanzania sh Milioni 31 Kwa vitu vyote.
Vitus ameongeza kuwa wao kama Kampuni wamekabidhi mahitaji hayo hivyo viongozi husika ndio wataoana wanagawaje lakini wameelekeza kwenye kata mbili ambazo ni ,kata ya mto wa tembo , na kata ya shambalai.
" Kama Kampuni tumetoa Kwa ujumla ila wao ndio wanajua namna watakavyogawanya chini ya usimamizi wa mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo husika "Amesema Vitus
Pia Vitusi amewashauri wadau mbalimbali kuendelea kujitoa nakwamba wakati mwingine majanga kama hayo yanapotokea watu wanakuwa hawajajipanga hivyo nivema kujitoa katika kile kidogo unachokuwa nacho na wao kama wawekezaji wamejitoa baada ya kuguswa kutokana na kile kimejitokeza.
Meneja huyo ametoa wito Kwa watanzania kuendelea kuendeleza umoja wetu kama watanzania na hasa yanapotokea majanga kama hayo kusaidia pale mtu anapoweza ili watanzania wenzetu kuweza kupata nafuu kutokana na changamoto husika .
Amesema kuhusu Serikali hasa ngazi ya Wilaya imefanya kazi kubwa sana ya kuhakikisha wahanga hao wanapata mahitaji ya kibinadamu na kwasababu Serikali haiwezi kufanya Kila kitu kwahiyo nao wao kama wadau wameweza kutoa mchango wao huo ili kuweza kuunga mkono jitihada za serikali kuweza kuhudumia watu wake .
Akimzungumzia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuweza kukatisha ziara na kurudi haraka nchini kuungana na watanzania wengine ,Vitusi Amesema Rais Dkt Samia kama anavyofahamika Yeye ni mtu wa watu kwakweli na amedhihirisha hilo tangu alivyoingia madarakani.
Amesema Rais ni mama anayejali watu wake na nikweli amekatisha ziara hiyo ili kuja nyumbani na kuona watu ili kujua ni namna gani anaweza kusaidia hivyo na wao kwa kutambua jitihada hizo za Rais walikuwa hawana namna zaidi ya Kumsapoti Rais Dkt. Samia na ukizingatia Yeye ni mtu ambaye anawajali sana wawekezaji hususani wawekezaji wazawa.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo Simanjiro Christopher Ole Sendeka ameipongeza kampuni ya Franone mining and games kwa kuwachangia wahanga wa mafuriko hayo
Sendeka amesema kampuni hiyo imekuwa msaada mkubwa kwenye jamii kwani hivi karibuni wakati wa ukame ilisaidia chakula kwenye shule mbili zilizokuwa zinakabiliwa na uhaba wa chakula zilizopo kata ya Naisinyai
Ameongeza kuwa kampuni ya Franone mining and games limetedi tunaishukuru kwa mengi pia mlisaidia shilingi milioni 60 kwa kata za endiamtu na Naisinyai na mmetumia shilingi 140 kwenye jamii yetu hongereni kwa moyo wenu wa upendo", amesema Sendeka.
Naye kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Asia Ngaliwason ameishukuru kampuni hiyo na kuwahakikishia kwamba msaada huo utafika kwa wahusika waliokumbwa na mafuriko
Asia ameongeza kuwa waliokumbwa na mafuriko ni watu 126 na watapata msaada huo katika kata za shambarai na kata ya msitu wa Tembo kwenye kayaa 49
Mwisho
0 Comments