DC ATAKA VYUO VYA UTALII VIKIDHI SOKO LA USHINDANI ,AKIPONGEZA CHUO CHA VOLCANO WAHITIMU WAMALIZA NA AJIRA MKONONI

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Vyuo vya Utalii hapa nchini vimetakiwa kutoa wahitimu bora wenye viwango vya kimataifa ili kukidhi soko la ushindani katika sekta ya utalii


Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Felician Mhehengerwa wakati alipohudhulia mahafali ya 5 ya ngazi ya cheti katika chuo cha utalii cha Volcano kilichopo Sakina jijini Arusha ambapo jumla ya wahitimu wapatao 87 wa fani mbalimbali ikiwemo utalii,Mapishi,Ususi,Fundi Umeme na Magari walihitimu na kutunukiwa vyeti.


Mkuu huyo wa wilaya pamoja na kukipongeza chuo hicho kwa namna kinavyotoa elimu na ujuzi, alisema jitihada zaidi zinahitajika kumudu ushindani katika sekta hiyo kwa kutoa wahitimu bora wenye viwango vya kimataifa.

"
Hivi sasa Mkoa wetu,tumepiga hatua sana kwenye utalii leo hii hoteli zetu zimejaa,  zinahitaji wahudumu wenye weledi na viwango vya juu vya kuhudumia watalii, lakini hapa Arusha bado viwango vya wahudumu havijakaa kiushindani"

Alisema changamoto hiyo itamalizwa na vyuo iwapo vyuo hivyo vitabadili ifundishaji na kujikita kwenye ubunifu wa kimataifa ikiwemo kufundisha suala la Lugha za kimataifa ili kwendana na soko la ushindani  duniani.

Aidha alitoa rai kwa wahitimu kuitumia elimu walioipata , kwenda kufanya ubunifu wenye tija na hadhi ya kimataifa ,namna ya kuanzisha na kuendesha  biashara kwa kiwango cha tofauti kwa kujua wanalenga nini ili kukidhi mahitaji ya wateja wao .

Awali Mkuu chuo hicho  ,Lazaro Thobias alisema chuo cha Volcano kimejikita kuzalisha wahitimu wenye viwango vya juu na wengi wa wahitimu zaidi ya asilimia 90 tayari wapo kwenye soko la ajira katika sekta mbalimbali mkoani hapa.
"Sisi chuo cha Volcano tunawaandaa vijana vizuri kwa kuwafundisha  ujuzi unaoendana na teknolojia za kimaiaifa na wanaweza kufanya kazi popote duniani kwani tunawafundisha pia lugha mbalimbali za kibiashara za kimataifa"

"Vijana wetu katika soko la ajira tumewaandaa vizuri ambapo wanaweza kutumia kompyuta hivi sasa dunia imehamia kiganjani na tehama kwa ujumla"Alisema Thobias. 

Baadhi ya wahitimu, Charles Wambura mhitimu waongoza watalii na Rahma Dickson aliyehitimu Mapishi walisema elimu walioipata imewasaidia kuwa na uelewa wa masuala ya utalii na kukishukuru chuo hicho kwa kuwapatia elimu bora na kwa sasa tayari wanaajiriwa.

"
Lengo langu ni kupata uzoefu wa kazi hapa nilipoajiriwa ila baadaye nakusudia kujiajili mimi mwenyewe ili jamii wajue kile nilichofundishwa nanufaika nacho kwa kufungua mgahawa wangu wa chakula"







Ends....




Post a Comment

0 Comments