CEDHA YAWANOA WAKUU WA VYUO VYA AFYA NCHINI ,KUHUSU CHANJO.

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA


Chuo cha Afya cha Cedha kilichopo jijini Arusha kimeendesha  mafunzo ya chanjo kwa wakuu wa vyuo vya afya na wakufunzi kwa lengo la kuimarisha huduma ya chanjo kwa wananchi ili kuzuia magonjwa yanayozuilika kwa njia ya chanjo . 


Akiongea wakati akifungua mafunzo hayo kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Dkt Omari Chande alisema suala la chanjo ni muhimu sana ,na linanlenga zaidi kwa watoto chini ya miaka mitano.

Dkt Chande alisema elimu hiyo ya chanjo kwenye vyuo ni umuhimu sana kwa sababu katika mitaala ya vyuo  vya afya ,elimu hiyo ilikuwa haifundishwi sana ila kwa sasa inapaswa kufundishwa ili elimu hiyo iweze kuenea  hasa kwa wanafunzi wanaohitimu katika vyuo hivyo .

"Mafunzo haya yamelenga Kuongeza uelewa na kuchukua ili elimu ya chanjo iweze kuenea, ni muhimu sana katika kuzuia magonjwa yanayoambukiza"

Awali Mkuu wa chuo cha Afya cha Cedha, dkt Johannes Lukumay alisema mafunzo hayo yamelenga vyuo vya afya vya serikali na binafsi na mashirika ya dini yalilenga kuimarisha sekta ya afya hapa nchini .

Alisema chanjo imesaidia kuongezeka kwa umri wa kuishi kwa mtanzania kufuatia uwekezaji mkubwa unaofanywa hapa nchini kwa kuwekeza zaidi katika sekta ya afya.

"Tuna wajibu wa kuhamasisha vijana wanaosoma vyuoni kuelewa umuhimu wa chanjo"






Ends..




Post a Comment

0 Comments