BENKI YA CRDB YAZINDUA MATUMIZI YA KADI ZA AMERICA EXPRESS HAPA NCHINI,ZITATUMIKA KWENYE MIFUMO YA MITANDAO YA ATM

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA


Benki ya CRDB  imeweka historia nyingine katika taasisi za fedha na mabenki hapa nchini baada ya kuzindua matumizi ya Kadi za America Express zitakazotumika kwenye mitandao ya ATM na Pos ya benki hiyo na hivyo kurahisisha utoaji wafedha kwa wageni mbalimbali duniani wanaoingia nchini.

Akiongea katika hafla hiyo iliyofanyika  katika hotel ya Gran Melia,jijini Arusha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ,Abdulmajid Nsekela alisema benki ya CRDB ni benki ya kwanza ya kizalendo kuingia ubia wa pamoja na America Express ili kumrahisisha mteja yoyote duniani kutumia kadi za America Express kutoa fedha kupitia mtandao wa ATM na Pos za  CRDB . 

"Benki yetu ya CRDB imekuwa ya kwanza kuanzisha huduma ya Tembo kadi,Viza na  master kadi na kuongoza katika ubunifu,ili uweze kumfikia mteja lazima utengeneze  mazingira mazuri na mepesi ya kupata huduma".

"Benki ya CRDB  tunajivunia  kwa wenzetu wa America Express kwa kuingia ubia wa pamoja kwa kuruhusu huduma hiyo ipatikane kwwnye mitandao yetu ya Pos na ATM, unapoamua na Mahusiano na America Express huyu ni mbia mkubwa sana duniani na benki yetu imetambuliwa kwa hilo"

Aidha kwa mwaka huu pekee  taarifa za Fedha za benki ya CRDB zinaonyesha kuwa takribani miamala Milioni 4 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 300 imefanyika kupitia mfumo huu.

Nsekela alisema huduma ya kadi za America Express zitasaidia  katika kuboresha na kuimarisha sekta ya utalii hapa nchini kwani watalii wengi wanatoka katika bara la America na CRDB imekuwa ya kwanza kutoa huduma Tanapa na Ngorongoro. 

"Ushirikiano huu unakwenda kuleta Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi nchini mfano katika mkoa huu wa Arusha ambao ni kitovu Cha Utalii wadau kama TANAPA, Ngorongoro, TATO na wengineo wataweza kunufaika na hudumu hii Kwa urahisi zaidi na tutaendelea kuwa wabunifu Ili kuweka mazingira mazuri na mepesi Kwa wateja"Alisema Nsekela

Akizindua Matumizi ya Kadi ya America Express katika hafla hiyo,Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela alisema ubia wa  America Express na crdb  utasaidia kuchochea uchumi katika sekta ya utalii baada ya watalii kutumia  kadi za America Express kutoa fedha kupitia mtandao wa ATM na pos za crdb.

Mongela alisema  benki ya CRDB imekuwa kiongozi kwenye mapinduzi ya  mifumo ya teknolojia ya kifedha hapa nchini inachochea  ukuaji wa kiuchumi,hapa nchini na kusema kuwa Serikali ya mkoa itaendelea kuunga mkono kwa sanabu amekuwa msau mkubwa wa maendeleo n kuzitaka taasisi zingine za fedha kuiga mfano huo.

"Kwa uzinduzi wa mashirikiano haya ya benki ya CRDB  na American Express utasaidia zaidi kuimarisha nafasi ya crdb kwenye maendeleo ya nchi yetu  katika kuwezesha mustakabali mzuri wa mfumo wetu wa kifedha."Alisema Mongela

Kwa Upande wake Makamu mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Profesa Neema Mori alisema kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza mapato na fedha za kigeni katika maeneo ya utalii hususan mkoa wa Arusha.

Alisema watalii wataweza kufanya malipo ya Serikali ikiwamo kulipia Visa na tozo nyingine stahili kwani mfumo tayari umeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa malipo ya Serikali GePG.

Kwa Upande wake Briana Wilsey, Makamu wa Rais, na Meneja Mkuu EMEA, Huduma za Mtandao wa Kibadilishanaji Kimataifa, American Express,alisema hadi Sasa wamefanikiwa kutoa kadi 130  katika nchi 90 duniani.

Briana alisema wameamua kushirikiana na CRDB Kwa kuwa ni benki inayokua kwa kasi ya hali ya juu,inatoa huduma nchi za maziwa makuu ambazo ni Tanzania ,Burundi na Congo,Mtandao mpana wa wadau na wananchama wake hivyo mashirikiano hayo yatataongeza mapato kupitia Sekta ya Utalii.







Ends...

Post a Comment

0 Comments