Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Benki ya CRDB imekabidhi gari jipya aina ya Vanguard lenye thamani ya Milioni 30 kwa mshindi wa jumla Dkt Bakati Zuberi akitokea Mkoani Arusha,aliyeshinda kupitia kampeni maalumu ya Benki ni SimBanking kupitia simu za mkononi.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi gari hilo ,iliyofanyika katika benki hiyo tawi la Usariver wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha wateja na biashara ,Steven Adil alisema benki ya CRDB ilitenga kiasi cha sh,milioni 350 kwa ajili ya kampeni hiyo iliyozinduliwa februali 14 mwaka huu,Mbagala jijini Dar-Es-salaam.
"Kampeni hiyo imekuwa na manufaa makubwa sana kwa watanzania wenye kufahamu huduma zetu za kidigitali zinazopatikana benki ikiwemo mikopo na akaunti"
"Tulikuwa na fedha thasilimu sh,milioni 350 ambapo kila wiki wateja 20 walikuwa wanaibuka washindi na kukabidhiwa kitita na fedha zote zimeshaenda kwa wateja"
Alisema kupitia kampeni hiyo benki hiyo ilitenga simu janja(smartphone) zipatazo 200 ambapo kila wiki wateja watano waliibuka washindi na kukabidhiwa simu zao,
"Wateja zaidi ya 500 wamefanikiwa kujishindia zawadi mbali mbali ikiwemo fedha thasilimu ,Magari,Laptop,Simu Janja hiki ni kitu kikubwa sana kwa benki yetu ya crdb na wateja wake"
Adili alisema mbali na zawadi hizo, crdb ilikuwa na magari sita aina ya Toyota Crown na kila moja lilikuwa na thamani ya sh,milioni 22 ambayo yote wamepatiwa washindi wa benki hiyo.
Aliongeza kuwa benki ya crdb imeendelea kupata faida na kuwanufaisha watanzania, wamemshukuru rais Samia Suluhu kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji zikiwemo taasisi za fedha kuweza kufanya biashara.
Alisema SimBanking inauwezo wa kufanya miamala kwa asilimia 95 kupata huduma mbalimbali za kifedha kupitia malipo ya aina mbalimbali ikiwemo mikopo na imesaidia kurahisisha maisha ya watanzania na kukuza uchumi wa taifa na kuwataka watanzania kujiunga na huduma hiyo.
Kwa upande wake mshindi wa gari hilo,dkt Bakari Zuberi aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma hiyo ambayo imempa urahisi wa kufanya malipo mbalimbali na kumwondolea gharama ya kwenda benki kwa ajili ya huduma za kifedha.
Aliwashauri wateja wa benki hiyo kujiunga na huduma ya SimBanking na kuacha kuogopa makato kwani gharama za kufuata huduma za kifedha katika benki ni kubwa kuliko kutumia malipo kupitia SimBanking.
"Baada ya kushinda watu wengi sana walinipigia simu kutaka kujua nimeshindaje, ila mimi nataka niwaambie siri ya ushindi wangu nilikuwa natumia sana SimBanking na asilimia 90 ya malipo yangu yote natumia SimBanking "
........Ends........
0 Comments