WAZIRI ULEGA AZUIA BIASHARA YA NYAMA KUCHINJA MAJIKE, ATAKA SHERIA ISIMAMIWE, MWEKEZAJI ELIYA FOOD AMPONGEZA RAIS SAMIA KUFUNGUA SOKO LA NYAMA SAUD ARABIA, AWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA WA MIFUGO KUUZA MADUME YA MBUZI

 Na Joseph Ngilisho, ARUSHA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdalah Ulenga,amewaagiza wataalamu wa Mifugo na mazao ya mifugo nchini, kusimamia  sheria za mifugo ili kuhakikisha mifugo inayochinjwa kwa ajili ya biashara ya nyama iwe ni madume pekee na majike yanaachwa kwa ajili ya kuzalisha


Ulega ameyasema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha Nyama cha Eliya food  Overseas Ltd kilichopo Longido mkoani Arusha ,kilichojengwa katika eneo maalumu la mauzo ya nje (EPZ) na kueleza kuwa kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda viwili vikubwa Tanzania vilivyopata fursa ya kuuza Nyama katika soko la nchini, Saud Arabia. 


Alisema fursa hiyo imekuja kufuatia ziara ya rais Samia suluhu nchini  Saud Arabia kwa mwaliko wa Mfalme wa Said Arabia na miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni suala la biashara ya uwekezaji, ambapo rais Samia alifanikiwa kuishawishi nchi hiyo kununua Nyama kutoka Tanzania. 

Waziri Ulega alisisitiza kuwa suala la ubora wa nyama inayozalishwa hapa nchini ni kipaumbele cha biashara hiyo nje ya nchini  , hivyo aliwataka wataalamu kusimamia sheria hizo kwa kuhakikisha mifugo inayochinjwa ni madume pekee ili kunusuru vizazi kwa kuchinja majike. 

"Kwa Mara ya kwanza Tanzania tumefanikiwa kupata soko la kuuza Nyama Uarabuni baada ya rais Samia kufungua milango, walikuja wataalamu kutoka Saudi Arabia na kufanya ukaguzi wa viwanda vyetu  vitano vya Nyama hapa nchini, lakini viwanda viwili vya Eliya food na Tan choice cha Mkuranga ndio vilifanikiwa kuchaguliwa"

Aidha alisisitiza kuwa ,pamoja na kwamba sheria ya Nyama hapa nchini inasisitiza uchinjwaji wa  madume, pia soko la nchi hiyo linahitaji Nyama kutoka kwa mfugo dume. 

"Simamieni vema sheria hii kuanzia minada ya msingi, kule Uarabuni hawapendi Nyama kutoka majike(Ke) na wakigundua tunaendelea kupeleka Ke watakataa hili soko,mwacheni Ke abaki kuzalisha  na dume (Me)awe kwa ajili ya biashara ya Nyama,sheria hii ipo ni jukumu letu kuisimamia tu "

Awali mwekezaji wa Kiwanda hicho cha Eliya food, Shabir Virjee alimpongeza rais Samia kwa kufanikisha kufungua milango ya kuuza Nyama katika soko la nchi za Uarabuni ambapo kwa Miaka  Mingi Tanzania ilikosa soko hilo. 

Alisema changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni ukosefu wa madume ya Mbuzi katika kukuza soko la Nyama ,alisema nchi za Uarabuni wanahitaji zaidi nyama ya mbuzi kutoka kwa mfugo dume .

"Changamoto nyingine ni bei ya nyama ya Ng'ombe kutoka Tanzania, tunashindwa kusafirisha Nyama ya Ng'ombe kwenda  Uarabuni kwa sababu  nchi za India na Australia wanauza nyama ya Ng'ombe nchini humo kwa bei rahisi na hivyo kuharibu somo la Nyama"

Katika hatua nyingine Virjee, ameiomba serikali kuwaruhusu kuuza soko la ndani tani 15 ya Nyama ambayo haiwezi kusafirishwa kwenda nje ya nchi iliyotokana na masalia  . 

"Tuna tani 15  ya Nyama( reject) ambayo tunayo kiwandani ambayo haiwezi kusafirishwa nje ya nchi na hii Nyama ilitokana na baashi ya mifugi kulalia upande kwa muda mrefu au kupata majeraha ya aina yoyote ikiwemo kupigwa"

Hata hivyo waziri Ulega alipokea ombi hilo na kumtaka mkurugenzi wa kiwanda hicho kuiandika barua serikali na kuielekeza kwake ili aifanyie kazi ikiwemo ombi la kusamehewa ushuru waweze kuuza kiasi hicho cha Nyama katika soko la ndani kuliko kiteketezwa kwa moto. 

Ends..... 













Post a Comment

0 Comments