WABUNGE EALA WAKERWA UTORO WA MAWAZIRI BUNGENI,MBUNGE ATAKA WAJADILIWE "WAPO MAWAZIRI HAWAJAWAHI KUHUDHULIA KIKAO HATA KIMOJA TANGU WACHAGULIWE " DKT TULIA APONGEZWA

 Na Joseph Ngilisho Arusha 

Wabunge wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki EALA,wamesikitishwa na mahudhulio duni ya mawaziri wa jumuiya hiyo wakidai hali hiyo inachangia baadhi ya hoja kukosa majibu na hivyo kukwamisha baadhi ya miswada inayojadiliwa.


Mbunge wa EALA dkt Abdulah Makame jana aliwasilisha hoja binafsi  katika kikao cha kwanza cha bunge hilo lililoanza kuketi jana na kuungwa mkono na wabunge wenzake akiliomba bunge hilo kijadili hoja ya mahudhulio hafifu ya mawazili.

Makame alieleza kusikitishwa KWAKE na mawaziri kujijengea utamaduni wa kukwepa vikao halali vya bunge hilo na kanuni ya 93 ya bunge hilo inawabana wajumbe wa bunge kuzingatia mahudhulio. 

"Ni bora bunge hili lijadili kwanza mahudhulio ya mawaziri wa jumuiya ya Afrika mashariki kwa sababu utoro wa mawazili bungeni ulisababisha mpaka pajeti ya jumuiya hiyo kuchelewa kupitishwa"
Dkt Abdullah Makame Mbunge EALA Tanzania

"Hata leo wakati bunge linaketi kwa kikao chake leo hapakuwa na waziri hata mmoja alikuwepo mwanasheria tu  na wapo mawaziri hawajawahi kuhudhulia hata kikao kimoja tangu wachaguliwe"

"Kitendo cha mawaziri kutohudhulia bungeni kinahudhunisha na kufedhehesha na kinaonesha wazi kwamba hawatoi umuhimu kwa shughuli za bunge na jumuiya letu"


Dkt Makame alisema kutohudhulia kwa mawaziri ni kuonesha dharau kwa bunge hilo na kuvunja moyo kwa waasisi wetu  wenye nia ya kutaka mtangamano uendelee lakini mawaziri hao wanaonesha kudharau mtangamano ulioasisiwa na wakuu wetu wa nchi.

Hata hivyo baada ya kuwasilisha hoja hiyo na kuungwa mkono na wabunge wengi spika wa bunge hilo  Joseph Ntakarutimana alimtaka mtoa hoja kwenda kuandaa vizuri hoja yake ili aiwasilishe  bungeni hapo na kujadiliwa .
Mashaka Ngole Mbunge EALA Tanzania

Naye mbunge ,Mashaka  Ngole kutoka Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya sheria,haki na hadhi za wabunge aliwasilisha ripoti ya marekebisho ya sheria ili wabunge watoe mapendekezo iwapo ipo haja ya kuzipitia upya na kuzifanyia marekebisho.

Alisema karibia idadi zote za kanuni zinapaswa kufanyiwa marekebisho ikiwemo kuanzisha kamati mpya za bunge ili kuleta ufanisi  na kwendana na wakati ,ukizingatia kwamba nchi wanachama zimeongezeka  tofauti na wakati jumuya hiyo inaundwa upya .

Katika hatua nyingine bunge hilo kwa kauli moja limepitisha hoja ya kumpongeza spika wa bunge la Tanzania Dkt Tulia Akson baada ya kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Rais wa mabunge duniani (IPU).

Hoja hiyo ililetwa bungeni hapo na mbunge wa Tanzania dkt Abdulah Makame akilishawishi bunge hilo kumpongeza spika Akson kwa kuliletea sifa na heshima taifa na nchi zote za jumuiya ya Afrika mashariki na afrikamkwa ujumla. 

Bunge hilo linaendelea nankika chake kwa kujadili hoja mbalimbali katika makao makuu ya jumuiya hiyo yaliyopo jijini Arusha.

Ends











Post a Comment

0 Comments