Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Wabunge wa bunge la EALA wametoa mapendekezo kwa nchi wanachama zisizotoa michango yao katika umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zichukuliwe hatua.Miongoni mwa wabunge walioleta hoja hiyo katika bunge la Tano linaloendelea makao makuu ya EAC jijini Arusha ni pamoja na mbunge kutoka Kenya Maina Karobia ambaye alisema kuwa nchi hizo zinapaswa kuchukuliwa hatua.
Alisema iwapo nchi hizo zinahoja ya msingi inayosababisha wao kutochangia ,zinapaswa kupeleka hoja zao katika bunge hilo au kwenye mkutano mkuu wa wakuu wa nchi wanachama EAC,ili hoja zao zijadiliwe kuliko kukimbia vikao vya bunge.
"Kama watu wanataka kutuambia wanamananizo katika nchi zao waje kwenye bunge ama wapeleke hoja zao kwenye mkutano wa wakuu wa nchi au baraza la mawaziri wa EAC kuliko kutoka nje ya bunge na kuongea huko kwenye mtaa, hakuna muungano bila pesa "
Alisema nchi ambazo zimekuwa hazichangii ziweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni na miongozo ya mikataba ya jumuiya hiyo ukizingatia kipengere cha 146 na 143.
Mbunge mwingine kutoka nchini Uganda, Paulo Msamali ambaye aliwasilisha hoja ya kutaka kujadili michango ya nchi 7 Wanachama alisema nchi ambazo zimeshalipa michango yao hadi sasa ni Tanzania,Kenya ,Uganda na Rwanda.
Alisema kila nchi wanachama inapaswa kuchangia takribani dola milioni 8 kila mwaka lakini nchi ya Sudani Kusini na DRC Kongo bado hawajalipa huku Sudani kusini ikidaiwa fedha nyingi za nyuma tangu imejiunga.
"Kwa Mfano mbunge mmoja anayetoka Kinshasa,Nchini DRC Kongo kuja Arusha kwenye bunge analipiwa tiketi ya ndege dola 3000 hadi 5000 na bado analipwa mshahara na fedha ya kujikimu wakati nchi yake haijachanga chochote"
Alishauri baraza la Mawaziri wa EAC kuwaambia wakuu wa nchi kuzishauri nchi hizo kulipa michango yao na kama hazita lipa ziondolewe ndani ya jumuiya hiyo.
"Kama hawataki kulipa wawatoe ndani ya jumuiya wanafanya nini na bado wanatoka ndani ya bunge na kususia vikao"
Ends..
0 Comments