Na Joseph Ngilisho Longido
Viongozi wa Mila wa Kabila la Kimasasi(Laigwanani) pamoja na viongozi wa dini wilayani Longido Mkoa wa Arusha,wamefanya maombi maalumu ya Kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kuliongoza Taifa hadi 2030 baada ya kufanikiwa kuifungua nchi kiuchumi.
Maombi hayo yamefanyika katika kijiji cha Mundarara wilayani humo na kuhudhuliwa na idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo na vijiji vya jirani huku wananchi hao wakiangua kilio na kuamsha mori wakitaka rais samia apewe nafasi ya kuongoza taifa hadi 2030.
Mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini aina ya Ruby ,Sendeu Laizer alisema kuwa uongozi wa Rais Samia umekuwa na tija kubwa kwa Taifa kutokana na mapinduzi makubwa ya kiuchumi aliyoyafanya katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya madini na amewajengea mazingira mazuri ya uwekezaji .
Alisema kuwa amani iliyopo hapa nchini imechangiwa na uongozi bora wa Rais Samia pamoja na serikali yake na umesaidia wawekezaji kufanya shughuli zao bila hofu huku akiwapa kipaumbele wawekezaji wazawa ambao wamekuwa walifanya vizuri kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa .
"Sisi hapa Longido ni wamoja na hatuna upinzani wa kisiasa na wananchi wote tunashirikiana kuleta maendeleo"
Akiongoza maombi hayo kiongozi wa Mila (Laigwanani)Peter Sengeyon alisema maombi ya watu waliokusanyika hapo yamelenga kumshukuru mungu kwa kumjalia afya njema rais samia na kumwomba mungu aendelee kumlinda kiongozi huyo aweze kuongoza hadi 2030.
Alisema Rais Samia ameletwa na mungu kwa makusudi ya kuisaidia nchi yetu hivyo lazima tumlinde na tumwombeee aishi na adumu kwenye uongozi wake hadi 2030
Naye mwenyekiti wa ccm wilaya ya Longido Papanakuta Mollel alimpongeza mwekezaji wa Mgodi wa Ruby Bilionea Sendeu Laizer kwa kuwekeza mgodi huo ambao umekuwa msaada mkubwa na umenufaisha wa wananchi wa kijiji hicho pamoja na halmashauri ya Longido kwa kukusanya mapato ya serikali.
"Sendeu amekuwa kiongozi mwema na mwadilifu anaisaidia sana jamii inayokuzunguka kwa kuwapatia ajira kuwajengea miundo mbinu ya barabara na shule ,mungu akubariki sana"aliseme na Kuongeza
"Nakupongeza sana Sendeu kwa mahusiano mazuri na wananchi wanaokuzunguka ambao umekuwa ukiwasaidia sana,pia nakupongeza kwa kuwa mlipakodi mzuri wa serikali pamoja na kusaidia maendeleo kwa jamii"
Naye mchungaji Daniel Kazimoto alisema maombi hayo yamfikie moja kwa moja rais Samia na kumpatia nguvu ya kusimama imara na kulitumikia taifa. Alimwomba mungu kumjalia afya njema rais Samia aweze kutawala hadi mwaka 2030.
"Watu wa Mundarara mungu ametupa nyota inayong'ara tumwombee rais wetu kila mtu kwa imani yake aombe hapa ili maombi haya yamfikie rais wetu Samia"
Ends...
0 Comments