Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Akiongea katika kikao kazi kilichoandaliwa na TRA ,Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha,Eva Raphael alisema kikao hicho kinalengo la kuwaongezea uwezo watendaji wa kata , Mitaa na maafisa Tarafa ili kupata taarifa sahihi za wafanyabiashara waliopo kwenye mitaa yao.
"Maeneo ya mitaa biashara nyingi zinafanyika katika maeneo ya watu naamini watendaji wanajua biashara hizo zilipo, hivyo watatusaidia kuziibua na kuwahamaisha wananchi kuona kodi ni wajibu wao kwa maendeleo ya ya nchi yao na sio hiari"
Naye katibu Tawala Mkoa wa Arusha,Missaile Musa aliwataka watendaji kuongeza nguvu katika kukusanya taarifa za wafanyabiashara wanaopaswa kulipa kodi ili kuongeza wigo wa walipakodi mkoani hapa.
Alisema kuwa mamlaka ya Mapato inawatukishi watache hivyo ni wajibu wa watendaji hao kuisaidia serikali kupitia TRA ili kuvuka malengo yao ya kukusanya kodi.
"Najua kuna vyanzo vingi vya kupata kodi kwenye mitaa Ikiwemo nyumba za kulala wageni tukisimamia vizuri ikiwemo kuziba mianya ya kukwepa kodi tunavuka malengo yetu kwa wakati"
Awali Mkurugenzi wa jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini amesema kuwa ofisi yake imejipanga kuwezesha ofisi zote za watendaji wa kata kwa kutoa nyongeza ya sh 500,000 kwa kila mwezi kwa ajili ya kusimamia upatikanaji wa mapato ya serikali
"Hii sh,laki tano tulioamua kuongeza kwa kila kata, sio kwa matumizi ya mtendaji pekee ,bali ni kuwezesha pia wataalamu kusaidia mapato na kwenye fedha ya maendeleo asiyefikia malengo hatapata bonansi"
Aliwaonya watendaji ambao wamekuwa wakichezea mifumo ya fedha kuwa hawatabaki salama kwani wengi wao wamefungwa kwa kujihusisha na mchezo mchafu wa kuiba fedha za serikali.
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho Grace Nyakaka afisa mtendaji wa kata ya Baraa alisema mafunzo hayo yatawasaidia sana kuwaongezea uelewa kwenye masuala ya kodi.
Naye mtendaji wa kata ya Murieth, polisi Buzela aliishukuru TRA kwa kuwaongezea uelewa na utambuzi wa masuala ya kodi ikiwemo kodi ya majengo ,ghala na maeneo ya Masoko na hivyo watashirikiana vema na TRA katika kuwatambua walipa kodi wapya.
Ends...
0 Comments