Na Joseph Ngilisho Arusha
Akiongea katika warsha ya siku moja iliyowahusisha wadau wa Mnyororo wa thamani wa sekta ya Nyama jijini Arusha,afisa wa TCCIA, mkoani hapa,Charles Makoi alisema kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia wadau wa Nyama kulalamikia huduma ya Nyama isiyoridhisha inayotolewa kwenye mabucha ikiwemo Nyama isiyokidhi viwango na ubora unaohitajika.
Charles Makoi ,Afisa TCCIA
Ritha Tarimo, Mkurugenzi TRIAS TANZANIA.
"Tunachangamoto ya wafanyabiashara wetu wa Nyama kutofuata miongozo ya usalama wa chakula ,miundo mbinu ya mabucha sio mizuri na ndio maana wadau wa nyama wanalalamika na sisi kama chama cha wafanyabiashara tukaonelea ipo haja kwa kufanya tafiti na kutoa warsha kama hii "Alisema utafiti huu ulifanikiwa kuwafikia na kuwahoji wadau wa Nyama wapatao 325 kati ya wadau 350 waliokusudia na kubaini kuwa mabucha ya kawaida ndio yenye kuuza nyama hafifu
" Tupo hapa kwa ajili ya kupata majibu ya utafiti wetu ili kwa pamoja tuweze kujadili na kupanga mikakati ya kubairesha mnyororo wa thamani wa sekta ya Nyama"
Kwa upande wake mshauri wa mradi kutoka Shirika la Trias Afrika Mashariki, Neema Kimaro alisema kuwa Trias Tanzania ni shirika la kimaendeleo linalofanyakazi na nchi 15 duniani ikiwemo nchi za Afrika mashariki chini ya mradi wake wa husisha kwa maendeleo endelevu kupitia wadau wake, wakiwemo TCCIA Arusha.
Neema Kimaro, Mshauri Mradi TRIAS.
Alisema utafiti wa nyama uliowezeshwa na Shirika hilo umepelekea kujua changamoto na fursa zilizopo katika sekta ya Nyama pamoja na mikakati ya kuboresha mnyororo wa thamani katika sekta ya Nyama.
"Shirika la Trias tunafanyakazi katika maeneo matatu matatu ambayo ni uhusishwaji,ujasiliamali,Mazingira na masoko "
Alisema katika utafili ukiofanywa Trias inapenda kuona zaidi uhusishwaji wa makundi mbalimbali unakuwepo katika mnyororo wa thamani wa nyama,pia wafanyabiashara wanafanyakazi zao katika mazingira rafiki,wanapata faida na kukuza biashara zao pamoja na masoko yanayofikika.
Alisema katika semina hiyo wadau walipendekeza mambo mbalimbali katika kuboresha mnyororo wa thamani ikiwemo matumizi ya teknolojia,usalama wa nyama,vitendea kazi ,elimu pia kipengele cha ushirikishwaji wa wadau katika utungwaji wa sera za nyama na tayari kikosi kazi kimeundwa kwa ajili ya kufanyia kazi mapendekezo hayo.
Naye mwakilishi wa bodi ya Nyama Tanzania,kanda ya Kaskazini,Rose Kamundi aliwataka wafanyabiashara wa Nyama katika jiji la Arusha kuzingatia sheria ya Nyama kwa kuuza nyama maeneo sahihi na yenye ubora unaohitajika kabla ya kumfikia mlaji.
Alisisitiza kwa wadau wa Nyama kuuza nyama bora iliyozingatia vigezo ikiwemo maeneo sahihi ambayo yameruhusiwa na bodi ya nyama kutoa huduma hiyo.
Alisema bodi ya Nyama ipo makini kuhakikisha usalama wa nyama kuanzia shambani hadi kwa mlaji na kwamba mabucha yasiyokidhi vigezo vya usajili yanafungiwa .
Ends...
0 Comments