TAZAMA PICHA YA KIBAKA MZOEFU ALLY DANGOTE ALIVYOTIKISA KWA KUMWAGA DAMU ZA WATU, ALIPANGA KUUA IDADI YA WATU KULIPA KISASA

Na Joseph Ngilisho, ARUSHA

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa ARUSHA limethibitisha kumuua kwa kumtwanga risasi Ally Dangote kibaka mzoefu mkazi wa Ungalimited ARUSHA ambaye amesumbua sana kwa matukio ya wizi mauaji na uhalifu wa muda mrefu. 
Ally Dangote Hatuko naye!

Katika kipindi cha Mwezi mzima Kijana Ally Dangote amekuwa akitafutwa kwa kutekeleza mauaji ya watu mbalimbali katika maeneo ya Longdong, Ungalimited na Sinoni

Kibaka mzoefu Ally Dangote kulia enzi za matukio yake ya uhalifu akiwa amefungwa pingu na mwenzake Hashimu Kibwerezi ,walikamatwa mwaka 2022. Picha hii niliipiga mwenyewe eneo la ESSO Agosti 8/mwaka 2022 wakiwa ofisi ya mtaa ARUSHA. 

Mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha leo wamejitokeza kushuhudia mwili wa kijana anayetambuliwa kwa jina la Ally Dangote (19) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, akidaiwa kutoroka baada ya kukamatwa.

Dangote kabla ya kutajwa kuhusika na matukio ya mauaji alikuwa rumande Magereza kwa muda mrefu kwa tuhuma za mauaji na hatimaye mwaka huu aliachiwa huru na Mahakama kutokana na kukosekana ushahidi lakini alikamatwa tena baada ya tuhuma za uhalifu mwingine.

Akizungumzia kifo hicho Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salvas Makweli amesema Dangote ameuawa baada ya kupata jeraha la risasi wakati akiwatoroka polisi.

"Ni kweli huyu mtuhumiwa alikuwa anasakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za wizi na mauaji na leo baada ya kuwekewa mitego tulimkamata na wakati anakwenda kuwaonesha wenzake aliruka kwenye gari na ndipo alipigwa risasi na kutokana na kuvuja damu nyingi alifariki akiwa hospitali," amesema.



Na Joseph Ngilisho Arusha, Agosti 8/2022

Vibaka maarufu hatari waliokuwa wakisakwa kwa muda mrefu wakihusishwa na matukio ya uporaji ,uvunjaji na wizi wa pikipili katika.maeneo mbalimbali jijini Arusha, wamenaswa wakiwa na  mali mbalimbali za wizi.

Katika operesheni iliyoendeshwa na polisi jamii wa mitaa mitatu ya Makaburi ya Banian,kanisani na Tindiga ilifanikisha kumtia mbaroni kibaka maarufu anayejulikana kwa jina la Ally Dangote(19) mkazi wa Unga limited jijini Hapa.

Operesheni hiyo pia ilimnasa mwizi hatari wa pikipiki Hashimu Kibwerezi(20)mkazi wa Osterbay ambapo baada ya kuhojiwa vibaka hao walikiri kujihusisha na matukio ya uporaji na kuonesha baadhi ya mali walizokuwa wakipora ambazo zimekamatwa.

Mwenyekiti wa kamati ya polisi jamii mtaa wa kanisani,Abubakari Seif alithibitisha kukamatwa kwa vibaka hao akidai ni mafanikio makubwa kwa kumnasa kibaka  Dangote kwani kwa muda mrefu aliwasumbua sana wananchi kwa  kupora na wizi wa vitu vyao nyakati za mchana na usiku.

Alisema kuwa mara baada ya kuwakamata na kuwahoji walikiri kujihusisha na matukio ya uhalifu katika maeneo ya Unga limited, Esso,Dampo, Ngusero kwa morombo na Uswahilini.

Selfu alisema kuwa vibaka hao walitoa ushirikiano na kuonesha bidhaa walizopora kwa kuwapelekea kwa watu waliodai ni madalali ambao wamekuwa wakishirikiana nao kutenda uhalifu huo.

"Baadhi ya vitu tulivyovikamata ni pamoja na Tv Flat scren 3,Tv moja ya kawaida,Deck 1,Sabufa 2 na Mota moja ya kusukuma maji"alisema.

Akiojiwa katika ofisi ya polisi jamii ,Mtaa wa kanisani ,kibaka Ally Dangote alikiri kujihusisha na matukio ya wizi na uporaji na kueleza kuwa pindi anapofanikiwa kupora huwa anapeleka hiyo mali kwa watu aliodai ni madalali na kuviuza kwa bei ya maelewano.

"Naitwa Ally Dangote nimekuwa nikiiba na kuvunja kila siku tangia nikiwa mdogo hadi sasa ,tumekuwa tukivunja milango na kuchukua bidhaa na kupeleka kwa madalali na tumekuwa tukiuza kati ya sh,80,000 hadi 200,000"alisema

Alisema yeye ni mwizi mzoefu na anawenzake ambao hushirikiana nao katika matukio hayo na kwamba amekuwa akipelekwa kituo cha polisi na kupelekwa gerezani lakini anapotoka huendelea na kazi yake kwa sababu hana kazi halali ya kufanya.

Akizungumzia njia anayotumia katika kutekeleza uhalifu anasema kuwa huwa anavizia na kuingia ndani kwa kasi ya ajabu pia nyakati za usiku au mchana huwa anavunja milango kwa kutuma  vifaa maalumu na kisha huingia ndani na kuiba na mara nyingi kazi hiyo huifanya akiwa peke yake ila kuna maeneo humlazimu kuwashirikisha wenzake

Kibaka mwingine Hashimu alikiri wizi wa pikipiki kwa kushirikiana na vibaka wengine aliodai hujulikana kama makonkodi ambapo wamekuwa wakivizia waendesha pikipiki na kuwapora majira ya mchana au usiku .

Mwenyekiti huyo alidai kuwa operesheni  ya kuwasaka vibaka wengine inaendelea na vibaka waliopatikana wamewakabidhiwa kituo cha polisi pamoja na vielelezo vyao kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baadhi ya wananchi walioporwa bidhaa zao,Sadi Hamadi na Vivian Kimambo wamepongeza hatua ya kukamatwa kwa vibaka hao akidai wamekuwa tishio katika makazi yao na kulitaka jeshi la polisi mkoani hapa kushirukiana na polisi jamii katika  doria maeneo yao ili kukabilia na na wimbi la vibaka kwakuwa hivi sasa wanaogopa hata kutoka nje usiku kwa kuogopa vibaka.

"Huyu Dangote  ni hatari sana kukamatwa kwake tunaomba jeshi la polisi wasimwachie ametutesa sana "alisema Vivian 

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo hakuweza kupatikana kuongelea tukio hilo.

Ends...










Post a Comment

0 Comments