Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Mwanamke huyo aliyejifungua Novemba 26,2023 kwa njia ya upasuaji ikiwa ni uzao wake wa pili ,watoto wake wote wana afya njema na uzito mzuri wa kilogram 1.4,1.5,1.8 na 1.9.
Akiongea hospitalini hapo Janeth aliishukuru hospitali hiyo kwa kumpatia huduma nzuri iliyowezesha kujifungua salama ikiwa ni uzao wake wa pili ukitanguliwa na mtoto wake wa kiume aliyemzaa mwaka 2015.
Alisema Mimba ya mapacha hao wa nne ilikuwa na changamoto kubwa ya yeye kuishiwa na damu,kuumwa mgongo na Kichwa na alipumzishwa kitandani tangu mimba ikiwa na miezi minne hadi kujifungua.
Mwanamke huyo alisema licha ya kukifungua salama lakini ana hofu ya kuwalea wanaye kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi katika familia yake na kuwaomba watanzania kumsaidia ili aweze kuwalea vizuri ikiwemo huduma ya maziwa.
Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Felician Mtahengerwa alisema serikali ya wilaya imeanza kuchukua hatua ya kumsaidia namna ya kulea watoto hao ikiwemo kuwakatia bima ya Afya na wadau mbalimbali wameonesha nia ya kusaidia malezi ya wapacha hao.
Naye mganga mfawidhi wa Hospital ya rufaa ya Mt Meru,dkt Alex Ernest alisema Novemba 26 majira ya saa 9 usiku mama huyo aliweza kujifungua salama kwa upasuaji na kufanikiwa kupata mapacha wanne wakiwa na afya njema.
Alisema suala la kujifungua mapacha wengi ni jambo la kawaida ambalo linatokea kwa nadra kutokana na histori za koo ama familia ama changamoto za uzazi .
Alisema hospitali hiyo inawapa kipaumbele wajawazito wakati wa kujifungua bila kudaiwa chochote ikiwa ni mpango wa serikali wa kuhakkkisha inapunguza ama kuondoa vifo kwa mama mjamzito.
Naye baba wa mapacha hao,Crey Julias ambaye anafanyakazi ya kibarua cha ujenzi alimshukuru mungu kwa mke wake kujifungua salama mapacha wanne ila alisema changamoto iliyopo mbele yake ni namna ya kuwalea watoto hao kutokana na kipato chake kidogo .
Hata hivyo alisema bado ana hamu ya kuendelea kupata watoto wengine na aliwataka watanzania kumsaidia ili kuweza kuwalea watoto wake mapacha wanne ambao kwa sasa ni mzigo mkubwa.
Ends...
0 Comments