Na Joseph Ngilisho Arusha
ALIYEKUWA Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole sabaya na wenzake wawili Sylivester Nyegu na Daniel Mbura wanatarajiwa kusomewa rufaa waliokatiwa na jamhuri Novemba 17 mwaka huu siku ya ijumaa baada ya mahakama ya rufaa Tanzania kuahirisha rufaa hiyo iliyokuwa isomwe leo kutokana na warufaniwa wawili kutokuwepo mahalamani .
Ahirisho hilo limetolewa leo na naibu msajili wa mahakama hiyo ya Rufaa Tanzania, Abeesiza Kaleyegeya
Baada ya Silvester Nyegu na Daniel Mbura kutofika mahakamani.
Katika rufaa hiyo Jamhuri Chini ya mwendesha mashtaka wa serikali, DPP inapinga hukumu ya mei 8 2022 iliyotolewa na mahakama kuu kanda ya Arusha iliyomwachia huru Sabaya ,Nyegu Na Mbura
Leo Mahakama hiyo ya Rufaa ilikuwa itoe hukumu ya rufaa hiyo iliyosikiliza wiki moja iliyopita hata hivyo Sabaya peke yake ndiye aliyekuwepo mahakamani huku wajibu rufaa wenzake wawili hawakuwepo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Novemba 17 mwaka huu siku ya ijumaa.
Naibu Msajili wa Mahakama ya rufaa ,Abeesiza Kaleyegeya alisema mahakamani hapo kwamba kesi hiyo inaahirishwa hadi siku ya ijumaa kutokana nabkukosekama kwa wajibu rufani wawili ambapo kisheria wanapaswa wawepo kama takwa la kisheria linavyosema.
Awali rufaa hiyo namba 231/2022 ilisikilizwa Novemba mosi mwaka huu kwa zaidi ya saa 6 na Jopo la majaji watattu wakiongozwa na Jaji Jacobs Mwambegele ,Ignas Kitusi na Leila Mgonya.
Jopo la mawakili wa DPP,wakiongozwa na wakili Chivanenda Luwongo, aliiomba mahakama kufanyia marekebisho hoja zao ambazo awali zilikuwa saba na kubaki tatu kudai kuwa Mahakama Kuu ya Arusha ilikosea kuwaachia huru wajibu rufaa.
Wakili huyo aliieleza kuwa Mahakama kuu kanda ya Arusha ambayo ni ya Rufaa ya kwanza ilikosea kusema kwenye kesi ya msingi iliyowakuta Sabaya na wenzake na hatia kesi yao haina mashiko kwa sababu shahidi namba mbili hakuulizwa maswali na wajibu rufaa namba mbili na tatu na kufuta ushahidi wao wote na akawaachia huru.
Sababu nyingine ni mahakama hiyo kusema usikilizwaji wa awali wa kesi ulikosewa kwa sababu wajibu rufaa wawili (Nyegu na Mbura),kuwa kuna vitu hawakusomewa wakati waliandika kwa maandishi kuwa wametimiza.
Alitaja sababu ya tatu kuwa ni Jamhuri haikuweza kuthibitisha kesi yao pasipo kuacha shaka,jambo ambalo alisema kesi hiyo ilitibitishwa pasipo kuacha shaka yoyote ambapo upande huo wa jamhuri walirejea ushahidi na vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa kwenye kesi ya msingi.
Aidha wakili huyo alieleza mahakama kuwa ushahidi wa shahidi wa pili wa jamhuri siyo ushahidi pekee uliowatia hatiani wajibu rufani hao na kuwa ushahidi wa mashahidi wengine na vielelezo viliwatia hatiani washitakiwa hao.
Mawakili wa mleta rufaa walisema kwenye kesi ya msingi walithibitisha mashitaka yote bila kuacha shaka,upande wa wajibu rufaa walisema kwamba hawakufanya hivyo huku wakidai kuwa walishindwa kueleza hata eneo lilipo duka,wakati hati ya amshtaka ikisema duka lipo mtaa wa bondeni baadhi ya mashahidi wakidai duka hilo lipo Soko Kuu.
Hata hivyo mawakili wa wajibu rufaa Mosses Mahuna, alipinga hoja hizo akirejea ushahidi uliotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Mahuna alisema hukumu ya rufaa ya kwanza ilikuwa sahihi na hakukuwa na mapungufu huku akidai kuwa utaratibu wa hoja za awali haukufuatwa ipasavyo na kuhoji ssbabu zilizowafanya upande wa Jamhuri kushindwa kufanyia marekebisho hati ya mashitaka.
Hukumu inayopingwa ilitolewa Mei 6, 2022, na Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, ambaye aliwaachia huru Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na mahakama ya hakimu mkazi Arusha Oktoba 15, 2021.
Wakati wa usikikizwaji wa rufaa hiyo mchuano ulikuwa mkali kati ya mawakili wa upande wa serikali na upande warufaniwa waliokuwa wakiongozwa na wakili Mosses Mahuna .
Rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa siku ya Ijumaa Novemba 17 na itajulikana mbivu na mbichi iwapo Sabaya na wenzake watabaki kuwa huru ama watarudi gerezani kutumikia kifungo chao cha miaka 30 kilichotolewa oktoba 15 mwaka 2021 na mahakama ya Hakimu mkazi iliyowatia hatiani chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo kutoka mkoani Geita.
Ends..
0 Comments