SABAYA AIBWAGA TENA SERIKALI ,ASHINDA RUFAA YA MAJAJI WATATU UMATI WAMSHANGILIA WAKIMWITA 'GENERAL'

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA                    

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wameshinda rufaa iliyokuwa imefunguliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), ya kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Mahakama hiyo imetupilia mbali Rufaa iliyokatwa na Upande wa Jamhuri, ikipinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, kumuachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela.


Hukumu hiyo iliyosomwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Abesiza Kalegeya, leo Ijumaa Novemba 17, 2023, imesema hakukuwepo na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, badala yake Mjibu rufani wa kwanza Lengai Ole Sabaya, alikuwa katika majukumu yake halali ya kufuatilia Makosa ya uhujumu uchumi kama ilivyoelezwa na Mashahidi wenyewe wa upande wa mashtaka. 

 

Mahakama hiyo ya rufaa iliyokaa chini ya Mwenyekiti wake Jaji Jacob Mwambegele imeeleza zaidi kwamba, Mahakama ya Hakimu Mkazi iliyomtia hatiani Sabaya na wenzake, ilikosea kutochambua  ushahidi unaoonyesha wazi kwamba, haiijawahi kutokea Jambazi akamate Mtuhumiwa, amnunulie Ndizi na baadae kumpeleka Polisi kama Mashahidi wenyewe walivyoelezwa kutendewa na Sabaya.


Majaji wameeleza hiyo ni aina ya kwanza ya unyang’anganyi wa Majambazi kuepeleka waliowaibia Mahakamani, na kuhitimisha kwamba Wajibu rufaa waliachiwa kihalali na Mahakama Kuu.


Mkurugenzi wa Mashtaka alikata Rufaa kupinga uamuzi wa Jaji E. Kisanya, kuwaachilia huru Lengai Ole Sabaya, Sylivester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha.


2nds..


Post a Comment

0 Comments