Na Joseph Ngilisho Arusha
Mchuano Mkali wa kisheria umeibuka katika mahakama ya rufaa Arusha,baina ya mawakili wa utetezi dhidi ya jamhuri katika kesi ya rufaa iliyokatwa na upande wa jamhuri wakipinga kuachiliwa huru kwa aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole sabaya na wenzake wawili.
Rufaa hiyo ambayo imesikilizwa leo Nov 1 2023 mbele ya majaji watatu wa mahakama ya rufaa wakiongozwa na jaji Jacobs Mwambegele,Ignas Kitusi na Leila Mgonya upande wa jamhuri unapinga uamuzi uliomwachilia huru Sabaya na wenzake .
Hata hivyo usikikizwaji wa rufaa hiyo umekamilika baada ya mvutano mkali wa kisheria uliodumu kwa saa 6 na uamuzi wa mahakama hiyo unatarajiwa kutolewa kwa tarehe itakayopangwa na pande zote zitajulishwa kupitia msajili wa mahakama .
Rufaa hiyo namba 231 ya mwaka 2022 ,Upande wa jamhuri unapinga hukumu iliyomwachia huru sabaya na wenzake iliyotolewa na mahakama kuu Mei 8, mwaka 2022 baada ya mahakama hiyo kubaini mapungufu katika mwenendo wa ushahidi.
Wengine walioachiwa huru na kukatiwa rufaa na jamhuri ni Sylivester Nyegu na Daniel Mbura
Katika mchuano huo uliotawaliwa na mabishano ya hoja ,ulichukua takribani masaa 6 kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 10.30 jioni ,ambapo upande wa utetezi uliongozwa na wakili kinara Mosses Mahuna ,walipambana kupangua hoja saba za waleta rufaa hadi zikabaki tatu baada ya kuzifanyia marekebisho.
Hoja zilizowasilishwa na warufani wakiongozwa na wakili wa serikali mkuu,Chivanenda Luwongo waliieleza mahakama hiyo sababu za kupinga kuachiliwa huru kwa washtakiwa ni kwamba mahakama ya kwanza ya rufaa ilikosea kwa kusema kesi yao haina mashiko kwa sababu shahidi namba mbili na tatu hakuulizwa maswali na wajibu maombi .
Alisema hoja nyingine ni kwamba mahakama hiyo kusema usikilizwaji wa awali wa kesi ukikosewa kwa sababu wajibu rufaa ambao ni Sylivester Nyegu na Daniel Mbura hawakusomewa baadhi ya vitu kwenye mwenendo wa kesi .
Akijibu hoja hizo wakili wa warufaniwa Mosses Mahuna alirejea kwenye ushahidi uliotolewa na mahakama ya hakimu mkazi Arusha akidai ndio msimamo wao kuwa hukumu ya rufaa ya kwanza ilikuwa sahihi na haikuwa na mapungufu.
0 Comments