Na Joseph Ngilisho, Arusha
Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Geoffrey Pinda ameitaka taasisi ya Wapima Ardhi na Tanzania (IST-AGM) kuwadhibiti na kuwachukulia hatua wapima ardhi na Ramani wasio na weredi wanaokiuka maadili ya taaluma yao kwa maslahi yao na kusababisha migogoro ya Ardhi isiyokoma hapa nchini.
Pinda ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa wapima Ardhi Tanzania (IST-AGM) na kuutaka mkutano huo wa mwaka kujitafakari na kujiwekea mikakati ya kuwadhibiti wenzao wachache wanaochafua taaluma hiyo kwa kukiuka maadili ya kazi .
"Wakati umefika wa kupitia chombo chenu na kubaini changamoto zinazowakabiri kwa sababu wizara yenu inakumbwa na migogoro mingi ya Ardhi inayoonesha udhaifu wenu katika kusimamia".Naibu waziri Pinda alisema kila kona hapa nchini ni vilio vya migogoro ya Ardhi ikiwemo mwingiliano wa mpaka kati ya kijiji na kingine,Kata na Kata ,wilaya na wilaya na Hata Mkoa kwa Mkoa na ni kutokana nabchombo chenu kukosa umakini.
Hata hivyo aliwapongea wataalamu hao kwa kuchangia maendeleo ya nchi kupitia miradi mikubwa na midogo ingawa changamoto ya vitendea kazi vya kisasa,ofisi bado serikali inaendelea kushughulikia.
"Nipende kuwaelez kuwa wizara yenu kwa sasa inajenga mfumo wa Tehama utakao wezesha kuwa na Ardhi Kiganjani yaani Ardhi app ambayo itatengeneza tiba ya kudumu kwa watanzania kuwa na Ardhi yao Kiganjani na kuondoa vishoka wanaosababisha migogoro ya ardhi "
Alisema Tume ya Ardhi imeonesha Mafanikio Makubwa katika zoezi la kuweka matumizi bora ya Ardhi ya vijiji na suluhishonya Mipaka ,hadi sasa vijiji 3000 vimepimwa na kuwekewa mipango ya matumizi bora ya Ardhi.
Awali Rais wa Taasisi ya wapima Ardhi Tanzania IST ,Tryphon Bilauri aliiomba serikali kuharakisha mchakato kufanyia mabadiliko ya sheria mbili zinazoongoza taaluma hiyo ambazo ni sura namba 324 iliyotungwa enzi ya mkoloni na sura namba 270 ya mwaka 1977 ambazo kwa sasa vifaa vya upimaji vimepitwa na wakati.
Alisema mabadiliko hayo ya sheria yataendana na matumizi ya teknolojia ya Upimaji Ardhi na kuandaa ramani na kuipa meno taasisi yao ya kuwez kuchukuliana hatua za kisheria.
Pia waliishauri serikali kuunda bodi Mathubuti ya kusimamia Taaluma ya upimaji wa Ramani kama bodi za taaluma zingine zilivyo ili kuepusha kuipatia serikali hasara.
Rais alisema mkutano huo umewakutanisha wapima Ardhi na wasanifu Ramani ikiwa lengo la mkutano huo ni pamoja na kujadoli mabadya teknolojia nq changamoto zake ba kuweka mikakati ya pamoja kukabiliana nazo.
Ends...
0 Comments