MCHUANO MKALI NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM ARUSHA , 83 WAREJESHA FOMU KWA KISHINDO , KATIBU CCM AONYA RUSHWA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA

JUMLA ya Makada wapatao 83 wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha wamerejesha Fomu za kuwania nafasi ya mwenyekiti wa ccm mkoani hapa iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti Marehemu ZELOTHE STEVEN ZELOTHE. 

Akiongea na vyombo vya habari baada ya zoezi hilo la kurejesha fomu kukamikika katibu wa ccm Mkoa ,Mussa Matoroka alisema kuwa jumla ya wanachama 88 walijitokeza kuchukua fomu lakini waliofanikiwa kurejesha ni 83.

Alisema mwitikio ulikuwa mzuri ikiwa ni haki ya msingi ya kila mwanachama mwenye sifa kugombea kwa ajili ya kukitumikia chama hicho.

Alisema taratibu zingine za kuchuja wagombea kulingana na sifa zao zitafanyika na mchakato wa kumpata mwenyekiti itatangazwa hatua kwa hatua.

Leo ndio mwisho wa kurejesha fomu hadi saa 10.00 jioni jumla ya wamachama 83 walirejesha fomu zao ,kiukweli mwitikio ni mkubwa kwa sabahu chama chetu ni kikubwa"

Aliwasihi wagombea wote wanaowania nafasi hiyo kutojihusisha na siasa za kupakana matope ikiwemo kucheza rafu na kutoa rushwa kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha nafasi ulioiomba.

Matoroka alipotakiwa kuwataja wagombea hao alikataa kwa kudai kwamba taratibu hazimruhusu hadi hapo mchakato utakapo malizika.

Nafassi ya kuchukua fomu ilianza juzi Novemba 21 hadi 23 ikiwa ni wiki tatu na siku kadhaa tangu kufariki kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo ZELOTHE STEVEN aliyefariki kwa maradhi Oktoba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.





Post a Comment

0 Comments