MAMA NTILIE NA MTEJA WAKE WAKUTWA UTUPU WAMEKUFA WAKIWA WAMELALIANA,POLISI WAVUNJA MLANGO WAKUTA JIKO LA MAHARAGE YAKICHEMKA

BY NGILISHO TV 

Mama Lishe aliyekuwa anauza katika mgahawa eneo la Mkwawa, Manispaa ya Iringa, Swiga Mwakalobo (35), pamoja na mteja wake, Jacob Chang’a; wamekutwa wamefariki ndani ya mgahawa huo huku miili yao ikiwa tupu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea kufanya uchunguzi zaidi.


Miili ya wawili hao imekutwa Jana Octoba 6, 2023 majira ya asubuhi, baada ya ndugu kumtafuta Swiga ambaye inadaiwa kuwa jana yake (Jumapili) usiku, hakuwa amerudi nyumbani.


Wakizungumza na Mwananchi baadhi ya majirani wamesema baada ya kubomoa mlango, wamesema walikuta miili hiyo ndani ya mgahawa huo, huku pembeni kukiwa na jiko la mkaa ambalo limebandikwa maharage.


"Hadi juzi usiku Swiga alikuwa akiendelea na shughuli zake za mgahawa na kwa sababu huwa anachelewa kufunga kutokana na maandilizi ya chakula cha asubuhi, hatukuwa na hofu," amesema Hamza Hamisi, ndugu yake Swiga.


Aidha Hamisi amesema kuwa, hadi kufikia jana asubuhi (Jumatatu), hawakuwa wamemuona marehemu Swiga na ndipo majirani walianza kufanya juhudi za kumtafuta kwa kumpigia simu bila mafanikio.


"Ndipo tukaenda mgahawani kwake na kupiga simu na tukasikia inaitia ndani ya mgahawa na mlango ulikuwa umefungwa. Tulipo chungulia tuliona miili miwili ambayo ilikuwa tupu," amesema Ibrahim Issa, mkazi wa Mkwawa.


Kwa mujibu wa Issa, waliamua kuvunja mlango huku wakidai kubaini wawili hao wakiwa tayari wamefariki.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Imalanongwa Hamis Chananja amesema walipiga simu polisi ambao walifika eneo la tukio.

Post a Comment

0 Comments