Na Joseph Ngilisho Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Felician Mtehengerwa amevitaka vyuo vya Afya nchini,kuzalisha wataalamu walio bora watakaosaidia sekta ya afya kuboresha huduma za matibabu nchini ili kupunguza wimbi la wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Aidha mkuu huyo wa wilaya alivitaka vyuo hivyo kutumia vifaa vya kisasa kufundishia wataalamu wa afya ili kuendana na teknolojia ya kisasa.
Mtahengerwa ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya vyuo vya afya kanda ya kaskazini yanayofanyika katika chuo cha afya Cedha jijini Arusha na kusisitiza kuwa, vyuo hivyo vizalishe wataalamu bora wa kutosha wenye kujali utu na afya ya Binadamu.
"Ivi kama watanzania wanaenda kutibiwa nje ya nchi na nyinyi ndo mnazalisha wataalamu mnajisikiaje ,mnafurahia kuona wanakwenda kutibiwa nje ya nchi???, mmajua serikali inatumia kiasi gani cha fedha kutibu watanzania nje ya nchi,siku mkijua hilo mtafundisha vizuri na kuzalisha wataalamu wazuri"
Alisema mpango wa serikali ni kuhakikisha watanzania wanatibiwa hapa nchini na ndio maana rais Samia Suluhu amewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika sekta ya afya ili kuwasaidia wananchi kupata huduma bora ya afya hapa nchini,lakini changamoto kubwa iliyopo ni kukosa wataalamu wa afya wa kutosha wenye kuthamini uhai wa binadamu ,weledi na wenye uhakika na kazi yao.
"Rais wetu amewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika sekta ya Afya lakini changamoto tulionayo ni wataalamu ,tunahitaji wataalamu bora kuweza kuhudumia vituo vya afya ,hospitali na zahanati ili tumalize wimbi la wagonjwa wetu kwenda kutibiwa India ,tunahitaji wagonjwa wetu watibiwe hapa nchini na wataalamu wetu"
Katika hatua nyingine Mtehengerwa alionya baadhi ya wafamasia ambao wamekuwa na tabia ya wizi wa dawa za serikali kwa kuchezea mifumo ya serikalj na kufanya udanganyifu ,akivitaka vyuo hivyo kwenda kuwafundisha vizuri ili waepuke tabia hiyo.
Awali mratibu wa Mafunzo hayo dkt Johannes Lukumay ambaye pia ni mkuu wa Chuo hicho cha afya cha CEDHA,alisema rais Samia ameipa kipaumbele sekta ya afya kwa kuwekeza fedha nyingi na kwamba tangia ameingia madarakani amejenga vituo vya kutolea huduma ya afya kutoka milioni 8 hadi milioni 11.
Alifafanua kuwa rais samia amejitahidi kuwasogezea karibu huduma za afya kwa kujenga hospitali 430 , vituo vya afya 1030 na maabara binafsi 1216 .
Aidha alisema rais Samia amewekeza huduma mbalimbali za afya ikiwemo ujenzi wa hospitali za rufaa katika mikoa ya Njombe, Songwe ,Geita ,Simiu na Katavi ,ambapo uwekezaji huo umegharimu kiasi cha sh, bilioni 891.5.
Alisema uwekezaji huo iwapo hakutakuwa na wataalamu wa kutosha ,utakuwa hauna manufaa, hivyo alitoa rai kwa vyuo vya afya nchini kuzingatia suala la kutoa wataalamu bora .
Alisema Rais Samia anatoa kiasi cha sh bilioni 16 hadi 20 kila mwezi, kuhakikisha dawa zinapatikana hapa nchini kwenye Hospitali ,vituo vya Afya na Zahanati ili kuhakikisha huduma ya dawa inapatikana muda wote.
Naye mshiriki wa mafunzo hayo, mkuu wa chuo cha Afya na sayansi shirikishi mkoani Kilimanjaro,dkt Elisante Muna alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uwezo na kuimarisha huduma za afya ili kutoa wataalamu bora watakaokidhi mahitaji ya watanzamia.
"Tunashukuru serikali kwa kuelekeza nguvu katika kuboresha sekta ya afya mambo mengi ambayo tulikuwa hatufanyia hapo awali hivi sasa yanafanyika hapa nchini, hususani matibabu ya moyo,upasuaji wa kurekebisha maumbile na mengine mengi"
Tunatarajia baada ya semina hii kwenda kutoa wataalamu bora zaidi walio wengi "
Ends...
0 Comments