Na Joseph Ngilisho Arusha
Waliikuwa wafanyakazi zaidi ya 400 wa shamba la Maua la Kilflower wamezingira jengo la ccm mkoa wa Arusha muda huu, wanadai malipo yao zaidi ya bilioni 3 kutoka kwa mwajiri wao ambaye kwa sasa hayupo ila serikali iliwaahidi kuwalipa ,wamesema watalala hapo mpaka kieleweke .
Hakuna kiongozi yoyote hadi sasa aliyefika kuwasikiliza tangu wamefika katika jengo hilo majira ya asubuhi,wanataka Rais Samia Suluhu asikie kilio chao kwa sababu jambo hili analifahamu na aliwahi kuiagiza wizara ya fedha iwalipe lakini hakuna kilichoendelea hadi sasa ni zaidi ya miaka mitano wanadai.
0 Comments