BREAKING AJALI ZA NDEGE ABIRIA 60 HOI ,NDEGE MOJA INAWAKA MOTO

 By Ngilisho Tv BREAKING


Zaidi ya Watu 60 wenusurika kifo kwenye ajali ya ndege mbili tofauti zilizotokea katika Uwanja wa Ndege wa Kikoboga uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limethibitisha kutokea kwa ajali zote mbili za Ndege ambazo zimetokea kwa wakati tofauti leo.
TANAPA imesema Ndege ya kwanza ya Unity Air 5H-MJH aina ya Embraer 120 majira ya saa 3:40 asubuhi ikiwa na Abiria 30, Marubani wawili na Mhudumu mmoja ikitokea Zanzibar ilipata tatizo la kiufundi wakati wa kutua kiwanjani hapo lakini kwa juhudi kubwa za Marubani na Maafisa wa kiwanja hicho hakuna madhara yaliyojitokeza ambapo Abira wote, Marubani na Muhudumu mmoja wako salama na wanaendelea na ratiba yao ya Utalii hifadhini.

Katika taarifa ya pili, TANAPA imethibitisha kutokea kwa ajali ya pili leoleo saa 9:30 alasiri ikihusisha Ndege ya Kampuni ya Unity Air 5H-FLM aina ya E120 ikiwa na Abiria 30, Marubani wawili na Wahudumu wawili iliyopata ajali wakati wa kuruka katika kiwanja hicho ikielekea Zanzibar ambapo hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa katika ajali hiyo ambayo chanzo chake bado hakijafahamika.

#Ngilisho Tv update#

Post a Comment

0 Comments