ALLY DANGOTE KIBAKA SUGU AZIKWA KIMYA KIMYA CHINI YA ULINZI WA POLISI,WALIOJIPANGA KUITEKA MAITI ILI WAIADHIBU WAPIGWA CHENGA YA MWILI

                            


Ally Dangote(20) leo amezikwa kimya kimya katika Makaburi ya manispaa Njiro, waliojipanga kuiteka Maiti waambulia patupu.

Kibaka mzoefu Ally Dangote aliyeuawa juzi baada ya kutikisa jiji la Arusha kwa matukio ya mauaji ya raia walio na hatia  ,mwili wake umezikwa leo kimya kimya katika makaburi ya Manispaa yaliyopo Njiro jijini Hapa.

"Amezikwa na watu wachache sana na wengi wao ni ndugu wa marehemu chini ya ulinzi wa jeshi la polisi."alisema shuhuda mmoja wa mazishi hayo.

Kabla ya mazishi hayo vijana kadhaa walisikika wakidai watauteka mwili wa marehemu  na kuutembeza mtaani na kuendelea kumpiga wakiwa nna madai kwamba hawaamini kama amekufa hadi waone mwili wake.

Post a Comment

0 Comments