ZARA TOURS YAIBUKA KINARA SEKTA YA UTALII NCHINI YANYAKUA TUZO NYINGINE NZITO KUTOKA FALME ZA KIARABU, TAZAMA MBWEMBWE ZA MAMA ZARA, AMSHUKURU RAIS SAMIA!


Na Joseph Ngilisho MOSHI 

Kampuni ya utalii ya Zara Tanzania Adventure ya mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa mara nyingine imetunukiwa tuzo ya utoaji  bora wa huduma  za uwakala wa utalii Afrika.


Tuzo hiyo  amekabidhiwa mkurugenzi wa kampuni hiyo Zainab Ansell baada ya kutambua mchango wake katika utoaji wa huduma bora za utalii kwa kiwango cha kimataifa.
Aidha Tuzo hiyo imetolewa na kampuni ya utalii ya  World Travel Award's usiku wa kuamkia Oktoba 15 mwaka huu katika Falme za kiarabu ambako mama Zara aliambatana na mwanaye Leila ambaye ni mmoja ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Tuzo hiyo sasa inaifanya Kampuni hiyo ya Zara Tanzania Adventure ya mjini Moshi kuwa Kampuni Bora ya Utalii Afrika kwa mara ya pili mfululizo ikifanya hivyo mwaka jana na mwaka huu ambako sherehe za utoaji wa Tuzo hizo zilifanyika nchini Dubai 
Akizungumza baada ya Tuzo hiyo katika makao makuu ya Zara tours  mjini Moshi, Mkurugenzi wa Zara tours,Zainab Ansell (Mama zara) amewashuruku wadau wote waliochangia mafanikio hayo ikiwemo Wizara ya maliasili na Utalii,Bodi ya Utalii pamoja na mamlaka ya Hifadhi za taifa Tanzania(Tanapa).

Pia alimshukuru rais Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza utalii kupitia video yake ya Royal Tour ambayo imesaidia kutangaza vivutio na kukuza utalii hapa nchini pamoja na mazingira wezeshi katika sekta hiyo.

"Sisi kama Zara tumepata tuzo hii kwa mara ya pili tukitanguliwa na mwaka jana na imetupa nguvu zaidi,tunashukuru mungu sana na tunamshukuru sana rais samia kupitia video yake ya Royal Tour  imesaidia kutangaza utalii hapa nchini"

Alisema kwa sasa anaelekeza nguvu zaidi katika kampeni yake ya "Twende Zetu Kilimanjaro" katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika ambako kundi kubwa la wageni wanatarajiwa  kupanda mlima Kilimanjaro kuanzia desemba tano hadi desemba 9 mwaka huu.

Kwa upande wake meneja wa Zara tours Rahma Adam alisema kuwa desemba 4 mwaka huu kampuni hiyo imepanga  kupandisha bendera ya Taifa katika mlima Kilimanjaro na pia watapeleleka tuzo hiyo ikiwa ni sehemu ya  kusherehekea maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika .

Naye afisa masoko wa kampuni hiyo , Nancy Ngotea alisema kuwa wamefurahi sana kupata tuzo hiyo kwani ni tuzo ya kidunia na wanapeleka mlima kilimanjro wanakaribisha watanzania wote kushiriki pamoja nao.

"Tunashukuru sana mama samia kwa juhudi zake za  kutangaza utalii kwa kushirikiana na wadau wa utalii toa pongezi kwa taasisi mbalimbali na wale wote waliopata tuzo hizo "alisema .

Kampuni hiyo ya utalii ya Zara  iliyoanzishwa mwaka 1987,Mwaka jana 2022  ilishinda  tuzo ya Humanitarian Award katika soko la kidunia mjini London nchini Uingereza.

Ends...



Post a Comment

0 Comments