Na Joseph Ngilisho Arusha
Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa Nyonga na Magoti bure katika hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center ALMC jiji Arusha,kupitia mpango wa mama Samia Love uliotekelezwa na madaktari bingwa kutoka nchini Marekani ,wamemshukuru Rais Samia kutokana na maendeleo yao mazuri na kumwomba huduma hiyo iwe endelevu ili kuwasaidia watanzania wengine wenye changamoto kama hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelewa nyumbani kwake na taasisi ya Samia Love inayoratibu huduma hiyo hapa nchini,mmoja ya magonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa Goti,Ester Mengowo mkazi wa Mbulu Mkoani Manyara.
Alisema kuwa ujio wa madaktari hao imekuwa faraja kubwa kwake kwani aliteseka kwa miaka miwili akitembea na magoti kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyapata kwenye magoti.
Alisema alitumia madawa ya aina mbalimbali bila kupata hafuu ila baada ya kutokea kwa madaktari hao na kumfanyiwa upasuaji aliona kama miujiza na sasa anamshukuru sana Rais samia Suluhu Hassan kwa upendo wake kwa wananchi kwani amepona na anaweza kutembea mwenyewe bila usaidizi.
"Kwa kweli mimi namshukuru sana rais Samia niliteseka sana kuanzia mwaka 2015 hadi 2023 nilikuwa kama bibi kizee usiku silali nameza madawa lakini maumivu hayaishi lakini nilipofanyiwa operesheni nilifunguka na sasa natembea kama kijana wa miaka 15"
Naye mnufaika mwingine wa huduma ya upasuaji, Faidha Mtwana Juma mkazi wa Ngusero jijini hapa alisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Nyonga kwa muda wa miaka 10 akiwa hajiwezi nyumbani kwake ila baada ya kufanyiwa upasuaji anaendelea vizuri na anaweza kutembea bila kusaidiwa.
"Namshukuru sana rais Samia baada ya kutuletea hao madaktari bingwa na kunifanyia upasuaji hivi sasa naendelea vuzuri naweze kutembea mwenyewe hadi barabarani kwani kipindi hicho nilikuwa mtu wa kukaa ndani kusubiri kuletewa kila kitu nikiwa na maumivu makali sana"
Alimwomba Rais Samia kupitia mratibu wa mpango huo wa Mama Samia Love, Lazaro Nyalandu kuwaleta tena madaktari hao ili kuwasaidia wananchi wengine wanaoteseka na maradhi kama hayo ambao hawakupata bahati ya kuonana na madaktari hao ili warudi tena hapa nchini kutoa huduma hiyo ili kuwapa unafuu wa maisha wananchi wengine"
Awali mratibu wa mpango wa Mama Samia Love ,Lazaro Nyalandu alisema wamefarijika kuona idadi ya wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji wanaendelea vizuri na huduma hilo imekuwa la mafanikio makubwa.
Alisema mpango wa rais Samia ni kuwasaidia wagonjwa wote wasiojiweza wenye matatizo ya nyonga na magoti hapa nchini na sasa wapo kwenye hatua ya kuwatembelea na kuona maendeleo ya wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji katika mikoa ya Arusha ,Manyara Singida ,Mwanza ,Dodoma na Dar Es Salaam.
Alisema kupitia mpango huo jumla ya wagonjwa wapatao 49 kutoka mikoa mbalimbali walifanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo ya ALMC na hivi sasa wanawatembelea ili kujua maendeleo yao kabla ya ujio wa kundi lingine la madaktari bingwa wa kike kwa ajili ya kuwasaidia watanzania wengine.
Naye kaimu mkurugenzi wa hospitali ALMC,Godwil Kivuyo alisema zoezi la upasuaji kwa wagonjwa wa nyonga na magoti lililofanywa na madaktari 60 kutoka nchini Marekani kwa kushirikiana na madaktari wa Hospital hiyo Agosti 12 hadi 27 mwaka huu lilifanyika kwa mafanikio makubwa.
Alisema hospitali hiyo inamshukuru sana Rais Samia kwa kufanikisha zoezi hilo lililowezesha watanzania 49 kufanyiwa upasuaji na wote wanaendelea vizuri.
Alisema mahitaji bado ni makubwa sana na wanaiomba serikali huduma hiyo iwe endelevu ili kuwasaidia wananchi wengi wanaosumbuliwa na aina hiyo ya magonjwa.
Ends...
0 Comments