Na Joseph Ngilisho Arusha
Mamia ya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha ,wafanyabiashara ,viongozi na wananchi, wamejitokeza kwa wingi makao makuu ya ccm Mkoa kusaini kitabu cha Maombolezi cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Marehemu ZELOTHE STEVEN na kueleza kuwa alikuwa kiongozi shupavu, mnyenyekevu mwenye kujali utu wa watu.
Miongoni mwa waombolezaji hao ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Felician Mtahengerwa ambaye alisema kuwa mkoa wa Arusha umempoteza kiongozi mwenye sifa zote za uongozi na alijua kulea,Kuongoza na kushauri .
"Tumempoteza kiongozi katikati ya watu aliwahi kushika karibia vyeo vyote vya Polisi ,pengo lake ni kubwa sana na hatujui litazibwaje"
Naye mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa CCM Wilaya ya Arusha Mary Kisaka alisema chama cha Mapinduzi kimepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Mwenyekiti,kwani alikuwa ni mtu mwenye umoja upendo na ustaarabu hakupenda maneno maneno na makundi ndani ya chama.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya jiji la Arusha,Maximilian Illanghe alisema kuwa msiba huu ni mkubwa na umegusa kila mtu ,alisema anamkumbuka marehemu kuwa alikuwa kiongozi mwadilifu ,asiyependa makuu na alifanikiwa kuwaunganisha watu na chama na alikuwa mwanasiasa mtendaji.
Wengine waliosaini kitabu cha Maombolezo ni Pamoja na Naibu Meya wa jiji la Arusha,Abraham Mollel , Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Arusha,Ally Juma Mwinyimvua(Ally Meku) Mfanyabiashara maarufu Arusha,Askofu dkt Philemon Mollel,Mwenyekiti wa uvccm wilaya ya Arusha Hassan Mndeme,Katibu wa uvccm Mkoa wa Arusha, Ibrahimu Kijanga na wengine ambapo kwa pamoja wamemlilia marehemu wakisema alikuwa kiongozi shupavu asiyeyumbishwa mwenye maono yake thabiti.
Awali Katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Arusha Saipulani Ramsey alisema mwili wa marehemu utapokelewa leo majira ya saa tisa alasiri katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha na baadaye utahifadhiwa katika chumba cha kujifadhia maiti( Mochwale) ya hospitali ya Rufaa Mt Meru.
Alisema Marehemu atapumzishwa katika Nyumba yake ya milele, Nyumbani kwake katika kitongoji la Olosiva kata ya Oloirien wilayani Arumeru siku ya jumatatu oktoba 30 mwaka huu 2023.Huku watu mashuhuri ,viongozi ,wanasiasa na watu wa kada mbalimbali wakitarajiwa kushiriki mazishi hayo.
'Hata hivyo kuna taarifa kwamba marehemu kabla ya kifo chake aliwahi kutamka kwamba mwili wake usiagwe'
Ends......
0 Comments