Na Joseph Ngilisho ARUMERU
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya [DCEA] kanda ya kaskazini kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Arumeru,imeteketeza shehena ya gunia 237 za bangi zilizokamatwa kwenye operesheni inayoendelea wilayani humo ,baada kukuta yamefichwa kwenye Korongo .
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuteketeza mihadarati hiyo,katika kata ya Maji ya chai wilayani humo, Mkuu wa Operesheni wa Mamlaka hiyo kanda ya kaskazini ,Innocenti Masangula alisema magunia hayo ya bangi yametokana na msako mkali wa nyumba kwa nyumba unaoendelea wilayani humo ,hata hivyo hawakufanikiwa kuwakamata wahusika .
Awali mkuu wa wilaya hiyo Emanuela Kaganda ambaye alishuhudia uteketezaji wa bangi hiyo alisema wilaya hiyo ipo kwenye mapambano kabambe ya kutokomeza dawa za kulevya na katika kipindi cha mwezi septemba na OKTOBA walifanikiwa kukamata jumla ya gunia 316 ya bangi na mbegu zake.
Alisema wakazi wa eneo hilo wamebuni njia mpya ya kuficha magunia hayo ya bangi kwenye korongo ama kufukia ndani ya mahindi jambo ambalo walifanikiwa kubaini magunia hayo yakiwa yamefukiwa kwenye mahindi na mengine kufishwa korongoni bila wahusika kuonekana.
"Gunia nyingine tumeziteketezwa shambani nyingine zimeteketezwa hapa,na tutaendelea na zoezi hili"
Ameongeza kuwa serikali imejipanga kutoa elimu juu ya dawa ya kulevya ikiwemo ulimaji wa zao mbadala ili waachane na madawa hayo.
"Hivi sasa wananchi wanaojihusisha na kilimo cha bangi hawahifadhi tena magunia ama viroba vya bangi ndani ya nyumba zao badala yake wanaficha korongoni ama kuyafukia chini ya magunia ya mahindi"
Baadhi ya vijana wanajihusisha na uvutaji wa bangi wilayani humo walidai kuwa wapo tayari kuacha utumiaji wa bangi kutokana na elimu wanayoipata juu ya madhara yatokanayo na mihadarati,japo baadhi Yao walisikitishwa kuona bangi hiyo ikiteketezwa.
"Ni kweli sisi vijana wengi unaowaona hapa tunatumia shada(bangi)ila kwa kuwa Serikali imeonelea inamadhara na sisi tutaacha kutumia ila tunaomba hao wanaolima washikwe ili bangi ipungue mtaani"alisema kijana aliyejitaja kwa jina la Msukuma the badlandi makazi wa maji ya Chai.
Ends...
.
0 Comments