SHEHENA YA BANGI YATEKETEZWA ARUMERU,WAKAZI WABUNI MBINU MPYA KUWAKABILI POLISI KILIMO CHA BANGI,DC ASISITIZA NI MSAKO WA UVUNGU KWA UVUNGU.

Na Joseph Ngilisho ARUMERU 

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya [DCEA] kanda ya kaskazini kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Arumeru,imeteketeza  shehena ya gunia 237 za bangi zilizokamatwa kwenye operesheni inayoendelea wilayani humo ,baada ya kukuta yamefichwa kwenye Korongo na kwenye magunia ya mahindi. 

 Innocenti Masangula (DCEA)

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuteketeza mihadarati hiyo,katika kata ya Maji ya chai wilayani humo, Mkuu wa Operesheni wa Mamlaka hiyo kanda ya kaskazini ,Innocenti Masangula alisema magunia hayo ya bangi yametokana na msako mkali wa nyumba kwa nyumba unaoendelea wilayani humo ,hata hivyo hawakufanikiwa kuwakamata wahusika . 
 Masangula alisema zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa baada ya kufanikiwa kukamata magunia 237 pamoja na gunia 310 za mbegu ya bangi na kuwataka wananchi kujiepusha na kilimo cha zao haramu la bangi na wawe mstari wa mbele kufichua wanaojihusisha na zao hilo .

Awali mkuu wa wilaya hiyo Emanuela Kaganda ambaye alishuhudia uteketezaji wa bangi hiyo alisema wilaya hiyo ipo kwenye mapambano kabambe ya kutokomeza dawa za kulevya na katika kipindi cha mwezi septemba na OKTOBA walifanikiwa kukamata jumla ya gunia 316 ya bangi na mbegu zake.
DC  ARUMERU,EMANUELA KAGANDA 
Alisema wakazi wa eneo hilo wamebuni njia mpya ya kuficha magunia hayo ya bangi  kwenye korongo ama kufukia ndani ya mahindi jambo ambalo walifanikiwa kubaini magunia hayo yakiwa yamefukiwa kwenye mahindi na mengine kufishwa korongoni bila wahusika kuonekana.

"Hivi sasa wananchi wanaojihusisha na kilimo cha bangi hawahifadhi tena magunia ama viroba vya bangi ndani ya nyumba zao badala yake wanaficha korongoni ama kuyafukia chini ya magunia ya mahindi"
Baadhi ya vijana wanajihusisha na uvutaji wa bangi wilayani humo walidai kuwa wapo tayari kuacha utumiaji wa bangi kutokana na elimu wanayoipata juu ya madhara yatokanayo na mihadarati,japo baadhi Yao walisikitishwa kuona bangi hiyo ikiteketezwa. 

"Ni kweli sisi vijana wengi unaowaona hapa tunatumia shada(bangi)ila kwa kuwa Serikali imeonelea inamadhara na sisi tutaacha kutumia ila tunaomba hao wanaolima washikwe ili bangi ipungue mtaani"alisema kijana aliyejitaja kwa jina la Msukuma the badlandi makazi wa maji ya Chai.

Ends...





.

Post a Comment

0 Comments