Na Joseph Ngilisho Arusha
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hi Mkoani Kilimanjaro Lengai ole Sabaya kesho anatarajiwa kupanda kizimbani katika mahakama ya rufaa Arusha chini ya Majaji watatu baada ya upande wa jamhuri kutoridhika na uamuzi wa kumwachia huru mshtakiwa wao.
Katika rufaa hiyo Jamhuri inapinga hukumu ya Mei 8, 2022 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, iliyomuachia huru Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura baada ya mahakama hiyo kubaini kulikuwa na upungufu katika mwenendo wa kesi hiyo, ikiwepo hali ya kutofautiana kwa ushahidi.
Rufaa hiyo namba 231/2022 inasikilizwa na jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Jacobs Mwambegele, Ignas Kitusi na Leila Mgonya.
Sabaya aliibwaga serikali mara mbili katika uamuzi uliotolewa na Mahakama ya hakimu mkazi na mahakama kuu na hivyo upande wa Jamhuri kutoridhika na uamuzi huo na kuamua kujipanga upya na kukata rufaa mahakama ya rufani ,shauri linalotarajiwa kuanza kusikilizwa
Awali Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Oktoba 15, 2021 katika kesi hiyo ya jinai namba 105/2021.
Hukumu anayoipinga DPP ilitolewa Mei 6, 2022 na Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma ambaye alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuona kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa shauri kwenye mahakama ya haki mkazi Arusha.
Mei, 2022 Mahakama Kuu kanda ya Arusha alimuachia huru Sabaya na wenzake wawili waliokata rufaa na kupinga kifungo cha miaka 30 jela katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
0 Comments