Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa jukwaa la majaji wakuu wa ukanda wa nchi za kusini na mashariki mwa Afrika utakaofanyika oktoba 23 hadi 27 mwaka huu na utafunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jijini Arusha .
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Mkutano huo wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) Jaji wa Mahakama ya Rufani,Dk,Paul Kihwelo alisema Jukwaa hilo la majaji wakuu hufanyika kila mwaka na awamu hii Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
Jaji,Kihwelo alisema pia mahakama imejipanga vema katika kuhakikisha inatatua masuala ya kibiashara katika nchi za Afrika na kusisitiza kuwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano huo majaji wastaafu kutoka Tanzania watashiriki mkutano huo.
Alisema mkutano huo wenye kauli mbiu "Wajibu wa Mahakama za Kitaifa katika Utatuzi wa Migogoro kwenye Eneo Huru la Biashara la Afrika(AFCFTA),Matumizi ya Teknolojia ya Kisasa ili Kuongeza Ufanisi katika Utoaji wa Haki" utahudhuriwa na majaji wakuu wapatao 16 katika mkutano huo unaolenga kubadilishana uzoefu na miongoni mwa jenda zitakazojadiliwa ni nafasi ya mahakama katika utatuzi wa Migogoro katika eneo huru la biashara Afrika pamoja na utumiaji wa teknolijia katika utoaji wa haki.
Alisema mafanikio mengine ni utoaji wa mafunzo kwa watumishi wa mahakama ili kuboresha ufanisi wa utoaji haki,lakini pia mfumo wa data wa kesi ambao unampelekea mwanachi kujua mwenendo wa kesi zilizoamuliwa mahakamani .
Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,Profesa,Elisante ole Gabriel alisema mahakama inajumla ya majaji 17,watumishi zaidi ya 6000,mahakama za mwanzo 960 za wilaya 135 huku nne zikiwa mbioni kujengwa ,mahakama za hakimu mfawidhi Mkoa 30 na mahakama kuu 19 ikiwemo mahakama za Rufaa
Lakini pia kabla ya mkutano huo utatanguliwa na kikao cha Watendaji Wakuu wa mahakama na kusisitiza kuwa Tanzania ni mojawapo kati ya nchizenye mshikamani baina ya serikali na bunge
Alisisitiza waandishi kuzingatia uzalendo wa nchi sanjari kwa kuzingatia mazingira ya kimahakama wakati wote wa Mkutano huo kuuliza na kuandika kwa usahihi habari hizo ikiwemo kujitolea na baada ya mkutano huo washiriki watakwenda kutembelea vivutio vya Utalii katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngororongoro (NCAA)
Awali jaji mfawidhi wa mahakama kuu Joachim Chiganga alisema kufanyika kwa mkutano huo hapa nchini kutaleta manufaa mbalimbali ikiwemo kukutanisha majaji wakuu kutoka nchi mbalimbali pamoja na kutangaza nchi yetu Tanzania na vivutio vyake.
Ends...
0 Comments