NAIBU WAZIRI ARIDHISHWA NA KASI YA MABORESHO KIWANJA CHA NDEGE ARUSHA, ADAI MABORESHO YATACHOCHEA UTALII NCHINI

Na Joseph Ngilisho,Arusha .

Naibu Waziri wa Uchukuzi David kihenzile ameeleza kuridhishwa na maendeleo, usimamizi na maboresho yanayoendelea kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Arusha ikiwemo jengo jipya la abiria na sehemu ya kuruka na kutua kwa ndege.


Akizungumza jana Jijini Arusha wakati alipotembelea kiwanda hicho ziara zake ya Kukagua Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania(TAA) .


Alisema Tanzania ni ya pili Kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani ambapo asilimia 80 ya watalii hupita kaskazini mwa Tanzania huku mkoa wa Arusha ukitumika kama lango la kuingilia hivyo kukamilika kwa upanuzi wa njia ya kuruka na kutua kwa ndege na kufika mita 1880 Toka 1680 za awali na sehemu ya kugeuzia ndege na jengo jipya la abiria vitachochea ongezeko la wageni na watalii.


"Sambamba na maboresho yanayoendelea Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya mambo mawili makubwa kuongeza eneo la kurukia ndege Kwa Mita 200 ambapo awali lilikuwa na Mita 1680 na Sasa 1880, ujenzi wa jengo jipya la abiria lililofikia asilimia 92, maegesho ya ndege yameboreshwa, mindombinu ya kuingia uwanjani na sehemu ya kugeuzia ndege ambapo sasa ndege kubwa zitatua katika kiwanja hicho" alisisitiza Kihenzile.


Alisema uwanja wa ndege wa Arusha unahudumia takribani watu 296,000 Kwa takwimu zilizopo sawa na miruko inayofikia 39,000 Kwa mwaka ,hivyo alisema ni kiwanja muhimu Kwa uchumi wa taiga letu kwani watalii wengi wanakuja hapa Kwa ndege zao binafsi hata za abiria wanakwenda kwenye vivutio vyetu vya utalii hasa hapa kaskazini ambapo ndiyo lango kuu la utalii.


"Unapozungumza kiwanja hiki Cha Arusha ndiyo kitovu Cha watalii Kwa ndege za saizi ya kati ukiacha ndege kubwa za kimataifa hivyo ukamilifu wa hili eneo la kurukia ndege ambalo Lina sehemu za kugeuzia ndege na Jengo la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria 1,000 Kwa mara Moja vitainua sana uchumi wa Arusha Kwa  kuongeza watalii zaidi na kuongeza Pato la taifa"



Pamoja na hayo alisema maboresho ya  eneo la  maegesho ya magari ambalo limekamilika kinachofanyika ni kuongeza uwezo wa jengo la abiria lenye sehemu ya kukaa abiria na VIP za kutosha, sehemu ya kuingia na kutoka abiria , ni jengo zuri na la kisiasa maana kulikuwa na jengo dogo ila maono ni makubwa ya kuhudumia abiria laki Sita Kwa mwaka.



Vilevile aliitaka mamlaka ya Viwanja vya ndege kuhakikisha miradi iliyobaki inakamilika mara moja ili iende ikahudimie watanzania na kuwataka changamoto zote ambazo ni za kiwizara na kiserikali ziletwe Wizarani haraka.


Naye Kaimu Meneja wa Kiwanja Cha Ndege Cha Arusha  Zaria Waziri  alisema jengo jipya la abiria linategemewa kukamilikwa mwezi wa 12 mwaka huu na limefikia asilimia 92 mpaka Sasa.


Alisema mradi wa ujenzi wa Barbara ya kuingia kiwanja, maegesho ya magari na ndege, na mfumo wa kupaki magari  vimeshakamilika hivyo wanategemea kupata watalii wengi zaidi ambapo jengo likikamilika litahudumia abiria 1,000 Kwa siku na laki Sita Kwa mwaka na wanategemea kuweka taa ili uwanja utumike masaa 24.


Ends..


Post a Comment

0 Comments