Na Joseph Ngilisho Arusha
Watendaji Wakuu wa Mahakama kutoka nchi 13 wanachama wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) wanatarajiwa kukutana jijini Arusha Oktoba 22, mwaka huu katika mkutano mkuu wa mwaka ambapo pamoja na mambo mengine utajadili utawala wa kisheria.
Akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha Watendaji Wakuu wa Mahakama wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) Profesa Elisante ole Gabriel ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, amesema maandalizi ya kikao cha watendaji hao yamekamilika na kitakuwa na ajenda juu tatu ikiwemo ajande ya kuongeza wanachama.
Aidha alisema ajenda za marekebisho ya katiba ya chama hicho ikiwemo uboreshaji wa vyanzo vya fedha, uboreshaji wa mtandao wa chama hicho, mikakati ya masuala ya fedha huku nchi 13 za umoja huo zitakazoshiriki mkutano huo ambazo ni Angola, Botswana, Lesotho, Zanzibar, Shelisheli, Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Eswatini, Zambia, Namibia na mwenyeji Tanzania.
Katika hatua nyingine Prof Gabriel alisema kuwa amejipanga kuhakikisha mahakama ya Tanzania inakuwa kivutio cha mahakama za Afrika ili nchi za nje zije kujifunza namna ya kuendesha mahakama kidigitali.
Alisema hadi sasa Tanzania imejenga mahakama ya mfano Afrika lililopo makao makuu Dodoma ambapo ikikamilika itakuwa mahakama ya sita kwa ukubwa duniani likiwa na majengo matatu ya nguvu.
Ends...
0 Comments